Monday, 30 September 2024

VIDEO:-KIBENA FC WACHAPWA NA WALIMA PARACHICHI ITULIKE FC KWA MIKWAJU YA PENATI

 https://youtu.be/nQ3SOPqCz18


HALMASHAURI YA WILAYA GAIRO WAJA KUJIFUNZA KILIMO CHA PARACHICHI NJOMBE MJI


 


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji njombe Mhe. Erasto mpete ameupokea ugeni kutoka Halamshauri ya Wilaya ya Gairo ambao umekuja kujifunza kilimo cha Parachichi katika Halmashauri ya mji njombe .

Akizungumza Septemba  30,2024 mara baada ya kuupokea ugeni huo  Mhe Mpete amewakaribishwa wageni hao ambapo amewaomba kutembelea mashamba mbalimbali ya wakulima wakubwa na walio fanikiwa kupitia zao hilo ili waweze kujifunza na  kuyapata yale ambayo wanatarajia kupitia zao .

Kwaupande wake Mhe. Rachel Nyangasi Diwani kata ya Chigelana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Gairo amesema lengo la kuja kujifunza kilimo cha parachichi Halmashauri ya Mji Njombe nikutokana na ubora ambao halmashauri ya mji aimekuwa ikitengeneza katika zao hilo hasa kwa kuzingatia ubora ,namna ya Kaunda mashamba ya parachichi na hatau mbalimbali za kuanzishwa kwa mashamba ya zao hilo hadi katika masoko .



Halmashauri ya wilaya ya Gairo wamekuja na wataalamu wa kilimo ,Biashara pamoja na  Waheshimiwa madiwani wa wilaya hiyo ambayo imekuwa ikilima mazao mablimbali hasa alizeti na mahindi.

Na Mwandishi wako Mario Mgimba 

0622467223

 


Sunday, 29 September 2024

KIBENA FC WACHAPWA KIPIGO CHA MBWA KOKO NA ITULIKE FC

 Mechi kati ya Itulike FC na Kibena FC imemalizaka kwa Mikwaju ya penati baada ya Dakika 90 kumalizika kwakufungana goli moja huku kwa Upande Kibena FC Ndio waliotangulia katotika Mchezo huo kwa goli safi kwa mpira uliofungwa na Revaldo Ntumba baada ya muda mfupi nao Itulike wakajibu mashambulizi kwa Goli murua kutoka kwa Luoneko Ng'ande lililo Mshinda golikipa wa Kibena FC na kuhitimisha dakika 90.

Ndipo Mikwaju yapenati ikamua ambapo Itulike wakashinda kwamikwaju yaPenati 5_4




ITULIKE FC NA KIBENA FC WAKABIDHIWA MPIRA /MSHINDI AJINYAKULIA KITITA CHA SHILINGI LAKI MOJA

 



Mbunge wa Jimbo.la Njombe Mjini Mhe. Deo Mwanyika ametoa  shilingi  laki moja kwa Mabingwa wa Mwanyika Cup kata ya Ramadhani huki  na Timu ya Itulike FC wakipewa  shilingi elfu hamsini na mpira mmoja mara  baada ya kushindwa kutamba mbele ya wenyeji wao Itulike FC kwa mikwaju ya penati 4_5.

Akikabidhi zawadi hiyo Septemba 29,2024 Katika Uwanja wa Itulike  kwa niaba ya Mbunge Emilia Mwangeni  Katibu wa Mbunge Jimbo la Njombe  amesema ushirikiano unaotokana na  michezo ndio chachu inayopelekea Mbunge Mwanyika kuendelea kuimarisha michezo Jimboni kwake puamoja na kuboresha miundombinu ya Michezo ambayo amekuwa akiipambania akiwa Bungeni kuhakikisha vijana wananufaika na Michezo kutokana na ajira nyingi zinazotokana na michezo.



Akiendelea kuzungumza katibu wa Mbunge Ndugu Emilia amewaomba Vijana hao kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa kuchukua fomu na kutia nia katika nafasi mbalimbali za Uongozi.

kwa Upande wake Mhe .Nikson Nganyange Diwani wakata ya Ramadhani amesema mashindano hayo yametamatishwa kwa kushuhudia mitanange huo wakukata nashoka ambapo amewaomba vijana na wananchi wa mtaa huo kushiriki katika michezo kutokana na fursa zinazopatikana kypitia Michezo.

Saturday, 28 September 2024

#Mpanzu Kujiunga na Simba ? CAF Wasemaneno....

 πŸš¨ MPANZU hataweza kuichezea Simba kwa sasa kutokana na kuchelewa dirisha la usajili ambapo Wekundu hao watamuongeza kwenye dirisha dogo litakalofunguliwa Desemba mwaka huu atakapoanza kucheza mashidano yote. 


Kanuni za CAF zinaruhusu mchezaji atakayetumika kwenye michuano wanayoisimamia lazima awe na leseni inayomuonyesha anacheza ligi ya nchi gani. Simba italazimika kutomtumia Mpanzu katika hatua ya makundi.


Friday, 27 September 2024

MPANGO KAZI KATA YA NJOMBE MJINI


 Afisa Mtendaji kata ya Njombe Enos Lupimo awaalika wadau wa kata hiyo kushiriki Kikao kazi cha maendeleo ya kata ya Njombe Mjini ambapo kutakuwa na kuwasilisha mpango kazi wa maendeleo kutafsiri  4R za Mhe Samia Suluhu Hassan

MAKUFWE UCHAGUZI UTAKUWA WAHAKI NA AMANI MAKETE

 



Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali za Mitaa katika Halmashauri ya wilaya ya Makete Wiliam Makufwe ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema ikitokea mgombea amepatikana mmoja atapigiwa kura ya ndio au Hapana na hakutakuwa na utaratibu wa mgombea kupita bila kupingwa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.


Makufwe ametoa kauli hiyo Septemba 26,2024 wakati akitoa mwelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024 mbele ya viongozi wa vyama vya siasa,Viongozi wa dini,wadau wa maendeleo katika halmashauri hiyo na kueleza kuwa utaratibu wa kupita bila kupingwa hautakuwepo na kwa viongozi walioko madarakani uongozi wao utakoma ifikapo Oktoba 25,2024 na kuanzia Oktoba 11 hadi Oktoba 20 mwaka huu zoezi litafanyika la kujiandikisha wapiga kura ili kupata orodha yao.

Katika uchaguzi huo amesema watendaji wa vijiji na kata ambao ni wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika maeneo yao hawataruhusiwa kuandikisha au kuandaa orodha ya wapiga kura na jukumu hilo watapewa wataalamu wengine na wapiga kura watatambuliwa kwa kujiandikisha katika vijiji vyao au kutambuliwa na wakazi katika eneo husika huku zoezi la fomu za uteuzi na kurejeshwa kwa wagombea litafanyika kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 7 mwaka huu katika kila kijiji na ofisi ya mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo Iwawa.

Mdau wa maendeleo wilayani Makete Egnatio Mtawa Mkurugenzi wa SUMASESU na Green FM ameshauri kutoa wagombea bora na kuepukana na kadhia ya rushwa katika uchaguzi ili kupata wagombea wanaoweza kuleta maendeleo katika Halmahauri husika bila kusahau kuwepo kwa mkazo wa hamasa itakayosaidia wananchi kijitokeza kwa wingi kugombea nafasi na kuchagua viongozi

Naye Jasel Mwamwala Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Njombe ametaka vyombo vya habari kupewa nafasi katika mchakato huo sambamba na kuwepo kwa usawa kwa vyama shiriki ushauri ambao msimamizi wa uchaguzi amesema watauzingatia.

Caastory Ngonyani Afisa uchaguzi wilaya ya Makete ameviomba vyama vya siasa kushirikiana nao katika mchakato huo na kwa wale watakao kiuka kanuni na kujihusisha na vitendo vya rushwa hawatasita kuwaondoka katika zoezi hilo.

MGOGORO WA ARDHI TANGA WAFIKA KWA RAIS DKT. SAMIA.

 MGOGORO WA ARDHI TANGA WAFIKA KWA RAIS  DKT. SAMIA. 



Na Denis Chambi, Tanga.


FAMILIYA  ya Marehemu Bakari Kidawa kutoka  wilaya ya Tanga Mkoani hapa wametua kilio chao kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Samia Suluhu wakimuomba kuingilia kati mgogoro wao mashamba kati yao na uongozi wa Halmashauri ya jiji la Tanga ambao kwa umedumu mrefu licha ya kufuatilia kwa zaidi ya miaka 10 lakini bado hawajapata mwarobaini. 


Wakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Jijini hapa watoto hao walieleza kuwa wamelazimika kumuomba Rais Dkt Samia kuingilia kati baada ya kukosa msaada kutoka kwa mamlaka mbalimbali  kuanzia ofisi ya ardhi , mipango miji ambazo zimeshindwa kuwapatia haki yao licha ya kuwepo na vielelezo vinavyoonyesha uhalali wao wa kumiliki mashamba hayo yenye ukubwa zaidi ya hekali 10 .


Akizungumza mmoja wa wanafamia hao Koja  Kidawa alisema kwamba mgogoro huo ulianza mwaka 1,996 hata kabla ya marehemu baba yao hajafariki ambapo Kamishna Mkuu wa Ardhi aliziagiza mamlaka za Tanga kuwasikiliza na kuona namna watakavyoweza kuwasaidia kuutatua.


Kwa mujibu wa Koja Kidawa alisema kwamba baadhi ya mashamba ya marehemu baba yako yalichukuliwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Tanga na baadhi ya wafanyakazi wa Serikali bila kuwa na ridhaa ya marehemu baba yao.


Alisema hata hivyo Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Tanga lilikanusha kutwaa maeneo yao bali walikiri kugawiwa maeneo hayo na Ofisi ya Mipango Miji ya jiji la Tanga baada ya kuomba maeneo hayo ambayo yanapakana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).


Aidha alisema baada ya kuona wanapigwa danadana na mamlaka za Serikali mkoani Tanga ambazo ni Ofisi ya Mipango Miji ya Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na Mkurugenzi wa Jiji hilo Dkt Frederick Sagamiko na hivyo kulazimika kwenda Jijini Dodoma kuona na Kamishna Mkuu wa Ardhi ambaye aliwaandikia barua mamlaka za Tanga kuwahimiza kulitatua suala hilo haraka iwezekanavyo.


Alisema hata hivyo viongozi hao wa Tanga akiwemo Afisa Mipango Miji na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga hawajaonyesha dalili za kutaka kuwasaidia ili wapate haki yao ambayo wanaidai na hivyo kulazimika kufika kwenye  vyombo vya habari ili kumuomba Rais Dkt Samia Suluhu kuona namna ya kuwasaidia kutokana na kukosa fedha za kufuatilia suala hilo.


“Katika mgogoro huu tulilazimika kwenda kuonana na viongozi wa mkoa wa Tanga akiwemo Afisa Mipango Miji, Mkurugenzi wa Jiji na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa lakini hawakuonyesha dalili zozote za kutusaidia ndio maana tukaona ni muhimu tukuombe Mhe Rais Dkt Samia Suluhu utusaidia suala hili “Alisema


Kwa upande wake Kidawa Bakari Kidawa alidai kwamba katika eneo lengine la kwao Mipango Miji ililigawa kwa Mmiliki wa Shule ya Prince and Princes anayetambulika kwa jina la CN Mushi.


Kidawa alisema kwamba familia hiyo ina matumaini makubwa na Rais Dkt Samia Suluhu kwamba suala lao litashughulikiwa mapema na kuweza kupata haki yao ya msingi


“Tunamjua Rais Samia Suluhu ni mama mwenye huruma na sisi kama wanawe tunaamini ataingilia kati suala hili ili tuweze kupewa haki yetu “Alisema Kidawa Bakari Kidawa ambaye ni mtoto wa pili wa marehemu.


Hata hivyo jitihada za waandishi wa habari kutaka kupata majibu kuhusiana na sakata hilo kwa mamlaka husika ziligonga mwamba baada ya wahusika akiwemo Ofisa Mipango Miji wa Jiji la Tanga Mussa ambaye alidai hawezi kuzungumzia suala hilo mpaka apate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Jijini pamoja na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Tanga .

BUWASA WAANZA UPANUZI WA MTANDAO WA MAJI

 BUWASA WAANZA UPANUZI WA MTANDAO WA MAJI


Zadi ya wakazi Elf Tatu miatano wamitaa Minne ya Miembeni,Idara ya Maji Kiliman pamoja na Butakale Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara wameanza kunufaika na Upanuzi wa Mtandao wa Maji baada ya kukosa maji kwa Muda mrefu.


Maeneo ya mitaa hiyo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Maji ambapo Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira (BUWASA) wameanza kuongeza mtandao wa maji kwa maeneo hayo.



Changamoto ya ukosefu wa Maji ya Muda mrefu katika mitaa Saba ya Miembeni,idara ya Maji Kiliman, Butakale imepata ufumbuzi baada ya kuanza Upanuzi wa Mtandao wa Maji  kwa wakazi wa mitaa hiyo.


Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi wa Maji Safi na usafi wa Mazingira(BUWASA) Ester Gilyoma amesema Serikali inahakikisha wananchi wake wananufaika na Mradi huo wa Maji na sasa mtandao huo utawafikia wakazi takribani 3500 katika mitaa minne Halmashauri ya Mji wa Bunda.


Utekelezaji wa mradi huo wa maji adhima ya DK Samia Suluhu Hassan kumtua mama ndio kichwani kuhakikisha changamoto ya ukosefu wa Maji inaondolewa



Je, maandamano ya Chadema yamefanikiwa?


 Msururu wa maandamano ya kusimamisha shughuli na kutikisa nchi kwa sehemu kubwa yalimaliza wakati wa utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wingi wa maandamano ya wakati huo – yalikifanya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupachikwa lakabu ya “Chama cha Maandamano” na wapinzani wao wa kisiasa, yaani chama tawala.

Kinachoshuhudiwa sasa ni matangazo makali ya maandamano lakini – maandamano yenyewe hayaji na uzito kama wa wakati ule. Kwa lugha nyingine unaweza kusema haya ya sasa ni ‘maandamano tepetepe.’

Lakini mwitikio mdogo, sio kipimo pekee cha kupima ikiwa maandamano yamefanikiwa au la. Na kabla hatujazama kwenye mjadala huo, kwanza tujiulize katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu maandamano.

Mwanasheria Rugemeleza Nshala, ambaye aliwahi kuwa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika ameiambia BBC, hatua ya polisi kuzuia maandamano si halali kwani Katiba ya Tanzania, inaruhusu kuandamana, kutoa hisia na kupinga vitu vinavyoonekana kuwa kinyume cha Katiba.

#SourceBBCSwahili

Kwanini kombora hili la masafa marefu linalosifiwa na rais Putin lilikataa kuruka?

 



Kuna uwezekano kulikuwa na ajali mbaya katika kituo cha anga za juu cha jeshi la Urusi, Plesetsk mnamo Septemba 20.

Watafiti na wataalamu wa OSINT wanaamini kwamba kuna uwezekano mkubwa lilikuwa jaribio lisilofaulu la kombora la masafa marefu la RS-28 Sarmat, ambalo inaonekana lililipuka kwenye silo. Kulingana na taarifa zilizopo, BBC imejaribu kuunda upya matukio hayo.

Picha za setlaiti zimeonesha shimo kubwa lililosababishwa na mlipuko katika upande mmoja wa mtambo wa kufyatua kombora hilo. Idhaa ya BBC nchini Urusi ilichunguza picha hizo za setaliti zilizochukuliwa mwezi Julai na Septemba 23 za eneo hilo. Zinaonyesha kuwa sehemu moja ya mtambo wa kufyatua kombora hili iliharibika vibaya

Kwa kuongeza, huduma ya NASA FIRMS , ambayo inafahamisha mara moja kuhusu moto mkubwa duniani kote, iliripoti kuwa mnamo Septemba 20, moto mkali ulionekana kwenye eneo hili.

#source BBCSwahili

Wanyama hatari kwa wanadamu duniani

 



Kuna takribani spishi milioni 1.2 kwa jumla, lakini ni mnyama gani hatari zaidi ulimwenguni? Au, kwa usahihi zaidi, ni mnyama gani anayeua wanadamu wengi zaidi?

Kama vile filamu nyingi za Hollywood zimeonyesha, wanyama hatari zaidi kwa wanadamu, ni pamoja na baadhi ya majitu makubwa zaidi ya asili, kama vile simba na mamba. Walakini, wanyama wengi hawana hatari sana kuliko vile unavyotarajia - papa, kwa mfano, huua wanadamu 70 tu kila mwaka.

Inashangaza kwamba viumbe hatari zaidi duniani mara nyingi ni vidogo zaidi na wana uwezekano mkubwa wa kuua kwa magonjwa, sumu na njia nyingine, badala ya meno yenye ncha kali.

Lakini ni kiumbe gani ndiye mnyama hatari kabisa ulimwenguni? Zijue 10 bora hapa chini.



Ingawa unaweza kuwa umekisia kwamba mfalme wa msituni, ambaye haishi msituni angekuwa juu zaidi kwenye orodha hii ya wanyama hatari zaidi ulimwenguni, simba bado ni mwindaji mkali ambaye hungependa kumharibu. Mngurumo wake wa 114dB unapaswa kuwa onyo vya kutosha.

Kwa kawaida hushambulia wakati wa usiku kwa kutumia makucha makali na kusababisha majeraha makubwa na kwa kuumwa na kung'ata mifupa na fuvu la kichwa, simba ni mnyama wa kutisha.

Paka hawa wakubwa huvizia mawindo yao katika vikundi vidogo, wakimzunguka mtu asiye na bahati kabla ya kukimbilia kuua.

#Source BBCSwahili.

Mlinzi wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 24, atachangamkia fursa

 


Marc Guehi amevutiwa na nia ya Liverpool kutaka huduma zake, Florian Wirtz halengwi na The Reds na Newcastle ipo katika mazungumzo ya kandarasi ya Anthony Gordon.

Mlinzi wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 24, atachangamkia fursa yakujiunga na Liverpool na sio Newcastle ambao wamekuwa wakimezea mate kwa muda mrefu. (Football Insider)

Liverpool hawana nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 21 kwa pauni milioni 100. (Echo).

Newcastle wanatatizika kuendeleza mazungumzo ya kandarasi na winga wao Muingereza Anthony Gordon, 23, ambaye alilengwa na Liverpool msimu uliopita wa joto. (Telegraph )


Trump na Zelensky kukutana huku wanachama wa Republican wakiwa na hasira

 



Trump na Zelensky kukutana huku wanachama wa Republican wakiwa na hasira

  1. Donald Trump amesema atakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini New York siku ya Ijumaa.

    Mgombea huyo wa urais wa chama cha Republican aliambia mkutano wa wanahabari kwamba wawili hao watakutana mwendo wa 09:45 ET (14:45 BST) katika jengo la Trump Tower.

    Mkutano huo unatazamiwa kuendelea licha ya ripoti za awali kuwa ulifutwa huku kukiwa na hasira kutoka kwa wana Republican baada ya Zelensky kutembelea jimbo muhimu la Marekani la Pennsylvania.

    Siku ya Alhamisi, Zelensky alikutana na Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris katika Ikulu ya White House kujadili "mpango wake wa ushindi", ambao anatumai utaishinikiza Urusi kukubali kumalizika kwa vita hivyo kidiplomasia.

    Soma zaidi:

  2. Naomi Campbell apigwa marufuku kuwa mdhamini wa shirika la kutoa misaada

    .

    Chanzo cha picha,Getty Images

    Mwanamitindo Naomi Campbell amepigwa marufuku kuwa mdhamini wa shirika moja la kutoa misaada baada ya uangalizi kugundua kuwa fedha za shirika hilo zilitumika katika hoteli za kifahari na kwa huduma za saluni.

    Uchunguzi wa Tume ya shirika hilo uligundua kuwa shughuli za maonyesho ya mitindo kwa ajili ya usaidizi hazikufanyika kwa kiasi kikubwa cha pesa kilichopatikana kama ilivyotakiwa.

    Badala yake zilitumika kwa ununuzi wa sigara na usalama wa Campbell na malipo mengine ambayo hayajaidhinishwa kwa mmoja wa wadhamini wenzake wa shirika hilo.

    "Nimegundua leo kuhusu ugunduzi huo, na nina wasiwasi mkubwa," Campbell, 54, aliliambia shirika la habari la AP.

    Aliongeza kuwa yeye sio mtu "aliyekuwa na udhibiti" wa shirika hilo la kutoa misaada.

    Ahadi za kuchangisha pesa hazijatekelezwa

    Amepigwa marufuku kujihusisha na shirika hilo kwa miaka mitano huku wadhamini wengine wawili, Bianka Hellmich na Veronica Chou, wakipigwa marufuku kwa miaka tisa na minne mtawalia.

    Wawakilishi wa mwanamitindo huyo wa Uingereza wamewasiliana na BBC.

    Uchunguzi uligundua kuwa malipo yasiyoidhinishwa ya jumla ya £ 290,000 kwa huduma za ushauri yalifanywa kwa Bi Hellmich, ambayo ilikuwa ni ukiukaji wa katiba ya shirika hilo.

    Ingawa Bi Hellmich alikuwa amependekeza kurejesha fedha hizo, wasimamizi wa muda walioteuliwa na Tume walifanikiwa kurejesha malipo kwa shirika hilo


Mamlaka ya Lebanon yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja

 Waziri wa mambo ya nje, Abdallah Bou Habib, amezungumza katika Umoja wa Mataifa na kusema nchi yake inavumilia mzozo unaotishia uwepo wake, na kwamba ilikuwa ni muhimu kuukomesha kabla haujafikia hatua ya kutozuilika.

Hezbollah pia imeashiria kuwa haiko tayari kurudi nyuma, na inaendelea kurusha makombora dhidi ya Israel.

Upande mwingine, Israel imesema itaendelea kuwalenga Hezbollah huku mazungumzo yakiendelea, katika mashambulizi ambayo tayari yameua mamia ya watu kote Lebanon na kuwalazimisha makumi ya maelfu kuyahama makazi yao.

Huku kukiwa na shinikizo kubwa hospitalini na idadi inayoongezeka ya wakazi waliokimbia makazi yao, mamlaka ya Lebanon inaomba kusitishwa kwa mapigano mara moja.



Mazungumzo ya kusitisha mapigano yataendelea huku mapigano yakiendelea - Netanyahu

 



IDF yadai kuwaua viongozi wengine wakuu zaidi wa Hezbollah katika shambulizi lililopita

Jeshi la Israel linasema kuwa viongozi wakuu waandamizi wa Hezbollah waliuawa wakati wa mashambulizi katika eneo la Beirut siku ya Jumanne.

Katika operesheni waliyoiita "Mishale ya Kaskazini" IDF hapo awali ilisema ilimuua mkuu wa makombora na Kikosi cha Roketi cha Hezbollah - Ibrahim Muhammad Qabisi.

Katika taarifa zake za hivi punde jeshi la Israel linasema wakuu wengine wa kundi hilo waliuawa , akiwemo naibu wa Qabisi.

Wakati hayo yakijiri aubuhi ya leo zimeshuhudiwa picha zinazoonyesha makombora juu ya Haifa yakizuiwa.

Mfumo wa kupambana na makombora wa Iron Dome wa Israel ulikatiza safari za makombora juu ya Haifa, yaliyofyatuliwa kutoka Lebanon.

IDF inasema baadhi ya roketi zimeanguka katika maeneo ya wazi.




#source bbc swahili

MAPENZI KAA LA MOTO MTOTO OSCA AZAMA PENZI NA JIMAMA

 Oskar alibakia kule chini huku akiwa ananitumbulia macho machozi yalimjaa katika macho yake na yalianza kumdondoka liviaaaaa aliniita huku akiwa ananyuka kunifuata! Mirac aliniweka nyuma ya mgongo wake hakutaka kabisa Oskar anisogelee! Broo huyu ni mwanamke wangu na tayari ana Mtoto wangu Oskar alimwelezea Mirac lakini Kwa bahati mbaya Mirac hakumuelewa Kwa sababu alikuwa hasikii kiswahili




🀸🏻‍♀️ baby tafadhari nakuomba twende ndani aliniambia Mirac alinishika mkono akawa amenitoa pale Kwa Oskar Kwa sababu Kila nilipomuona Oskar nilikuwa nashikwa na hasira Kali sana Juu yake! Tulielekea ndani Oskar tulimuacha pale nje na nilimuonya mlinzi asije akamruhusu Oskar kuingia ndani! tulimaliza part usiku mida ya saa nne baada ya Hapo Mirac na wenzake waliondoka kurudi hotelini Kwa ajiri ya kwenda kupumzika huko!
Mirac na marafiki zake walikaa huku Tanzania Kwa siku Tano baada ya Hapo walirudi uturuki Mimi nilibakia Tanzania kusubilia ndoa ya Daddy & Mommy! Baada ya ndoa ya wazazi wangu niliondoka kurudi chuoni Emre nilimuacha Kwa Mom Kwa sababu hawakutaka kabisa Mimi niondoke naye! Sikurudi Tena kuishi hostel niliendelea kukaa Kwa Mirac maisha yaliendelea Mirac alinivisha Pete ya uchumba aliwatuma wazazi wake wakaenda nyumbani kwetu Tanzania Kwa ajiri ya kuniposa! Ananipenda πŸ™ˆπŸ™ˆ Mimi ndo usiulize πŸ™ˆπŸ™ˆ baada ya wazazi wa Mirac kwenda nyumbani kwetu kuonana na wazazi wangu Daddy and Mommy walinipigia wakaniuliza kama kweli Niko tayari kuolewa niliwaambia tu wapokee posa Kwa sababu tayari Mirac amekwisha nivisha Pete ya uchumba! Wazazi wangu walipokea posa baada ya Mimi kuwa nimewaruhusu wao kufanya hivyo! Penzi letu Mimi na Mirac lilizidi kunoga Kila sikuπŸ’‹πŸ’‹Siku Moja ilikuwa ni usiku nilikuwa zangu jikoni na Mirac tunaandaa chakula mara simu yangu iliita ilikuwa ni namba ngeni nilipokea baada ya kuipokea ilisikika sauti ya kiume ni ya mtu ambaye simfahamu kabisa!
Alijitambulisha ya kwamba yeye ni Jerome na alikuwa anahitaji kuonana na Mimi nilijaribu kumhoji namba yangu katoa wapi aliniambia ya kwamba Kuna rafiki yangu mmoja ndo amempatia namba! Mmhhh nilionyesha msikitiko.... Baby mbona uko hivyo ulikuwa unaongea na nani kwani!? Aliniuliza Mirac! Baby Kuna mtu kanipigia kajitambulisha kuwa yeye ni Jerome lakini simfahamu na anataka niende nikaonane naye! Hebu nipatie namba yake! Mirac aliniomba nimpatie namba ya huyo Jamaa nilimpatia namba akawa amempigia!
""Hello aliongea Mirac ""
""Hello nani!?""
""Mirac Mme mtarajiwa wa livia umempigia mwanamke wangu mda si mrefu ukiwa unahitaji kuonana naye kwani wewe ni nani!?""
""Ahahahahahaaaa huyo ni demu wangu wa mda mrefu sana Jana nilikuwa Naye na hata leo nimemkumbuka nikaona nimpigie akiweza aje tujikumbushie mapenzi kama aliyonipatia Jana broo tafuta pesa mwanamke anatulizwa na pesa na siyo hizo kelele unazonipigia unajinadi kuwa huyo ni demu wako mbona akiwa na Mimi Huwa anakataa ya kwamba Hana mwanaume tafuta pesa boys wewe! Demu ni chaote huyo wahuni tunajimegea tu kisela hata Jana Mimi mbona nilikuwa Naye tumejiachia sana Jana na alinipatia Penzi 😝😝 aliongea yule Mr Jerome tena Kwa kebehi baada ya Mirac kuambiwa hivyo alianza kuichanganua Ile kauli ya kwamba mbona hata Jana Mimi nilikuwa naye' livia Jana uliniaga kuwa unatoka so ulienda kuonana na Jerome!? Aliniuliza Mirac! nilitoka kwenda shopping sikwenda kuonana na yeyote! Livia unanicheat!? No baby unajua kabisa Mimi siwezi kufanya hivyoπŸ₯ΉπŸ₯Ή vile naogopa kuachwa Tena Kwa mara nyingine nilijikuta machozi yameshaanza kunitoka nilimpigia Mirac magoti nikamwambia darling niamini siwezi kufanya hivyo kwako nakupenda et!
Mirac aliniangalia Kwa hasira aliunyanyua mkono wake akataka kunitia konzi lakini alijizuia baada ya Hapo aliondoka akaniacha pale jikoni peke yangu aliingia chumbani akavaa koti la kujikinga na baridi baada ya Hapo alielekea parking akapanda kwenye gari lake akawa ameondoka! Nilizima majiko haraka nikawa nimechukua gari ili niweze kumfuatilia Mirac nilimfuata nyuma nyuma Hadi katika lodge Fulani alishuka pale akawa ameagiza kinywaji kikali na kuanza kunywa bila kupumzika nilifika pale nikampigia magoti nilimwambia Baby tafadhari nakuomba uniamini nakupenda wewe peke Yako! Livia hata Kwa Yale yote niliyoyafanya kwako hauridhiki kipi ambacho sijakufanyia livia!? Kwanini unanisaliti liviaπŸ₯ΊπŸ₯Ί alinisogelea akaninyanyua pale chini Kwa hasira aliniambia Livia nakuchukia😒😒 Mirac aliongea Kwa hasira huku machozi yakiwa yanamtoka nililegea nafsi na roho nilitamani tu nife Kwa sababu kitu kuachwa sikutaka Tena kinitokee katika maisha yangu Mirac baada ya kuniambia vile alinisukuma nikadondokea chini hakujali Kabisa πŸ™Œ alilipia kile kinywaji alichokuwa kaishakiagiza baada ya Hapo alisepa akaniacha pale chini niliendelea kukaa na kulilia pale chini nilimuuliza Mungu kwani Mimi Sina bahati ya kupendwa milele mbona Kila anayekuja kwenye maisha yangu nikishakoleza tu upendo kwake ananiacha bila kujali ni maumivu kiasi Gani nitakayoyapata! Mwenyezi Mungu fanya kitu naomba unirudishie Mirac wanguπŸ˜₯ siko tayari kutengana naye!
nililia walinzi wa kule lodge walikuja wakanitoa pale chini wakanipeleka kwenye gari Yangu! Nilikaa huko ndani ya gari huku nikiwa najiuliza nirudi Kwa Mirac au nielekee wapi 😒πŸ˜₯ hata Ile gari niliyokuwa nayo usiku ule ni gari yake aliyonizawadiaga siku ya birthday yangu je niirudishe hii gari nyumbani kwake usiku huu lakini ananichukia sitakiwi kuonekana katika macho yake😒πŸ˜₯ nikiwa pale ndani ya gari langu simu yangu iliita nilivyoangalia anayepiga alikuwa ni Jerome nilipokea Kwa hasira na kuanza kumtirilishia matusi makali Sana! Jerome alicheka sana Aliniambia livia mpenzi kwenye gari ya bwana wako Kuna kitu nimekiweka Nina Imani ni lazima tu atakupatia! Kitu😰😰 kwenye gari ya Mirac!? Nilikata Ile simu haraka nikaondoka pale lodge kuelekea nyumbani kule Kwa Mirac! Nilifika getini nikabonyeza kengere kijana wa getini alikuja haraka kunifungulia niliingiza gari ndani nikaiweka parking baada ya Hapo nilitelemka kule ndani ya gari lakini kabla sijapiga hatua Mirac alinifuata pale!
Mirac alifika akanitupia barua usoni kwangu alinikamata Kwa hasira akaniambia livia Kwa hiyo hata ndani ya gari langu unathubutu kuacha uchafu kama huu!? zilikuwa ni barua mbili Moja ilionekana kutoka Kwa Jerome na nyingine ilionekana ni kama Mimi ndo niliyeandika Tena ilikuwa ni mwandiko kama wangu kabisa barua zile mbili ilionekana ni kama Mimi nilipokea barua kutoka Kwa Jerome Kisha namimi nikamwandikia barua ambayo Bado ilikuwa haijatumwa kwake! Nilihisi kupagawa baada ya kuzisoma zile barua nilikumbuka Jana ni kweli nilitoka na hiyo gari ya Mirac lakini mbona sikumpatia mtu yoyote lift ni nani huyo aliyeweza kuingiza barua kama hizi kwenye gari ya Mirac inamaana huu mchezo nilianza kuchezewa tangu Jana bila kujua chochote πŸ˜₯😰!
Mirac tafadhari nakuomba unipe muda tuongee et kweli nakuapia simfahamu huyu mtu na hata hizi barua Mimi sijaziandika et! Mirac alicheka Kwa uchungu aliyafuta machozi yake Kisha akaniuliza Livia kwani ni kipi ulichokihitaji nikashindwa kukutimizia!? Nilikupatia Kila kitu Livia😒😒 lakini unathubutu kuandika barua kumwandikia mwanaume mwingine barua kama hiyo Kwa hiyo hunipendi eh😰!? Nakupenda Mirac simfahamu Jerome simfahamu nakuapia babangu tafadhari nakuomba uchukue muda ulichunguze hili Mimi nahisi tu Kuna mtu ambaye ananifanyia mchezo mbaya nakuomba usiniache Mirac wangu usiniache nakupenda naomba usije ukaniacha et😰😰
Livia chukua Kila kilicho chako kwenye hii nyumba uondoke nakuchukiaaaa😰😰 sipendi usaliti katika maisha yangu! nilijaribu kujielezea lakini Mirac alikuwa na hasira sana hakutaka kabisa kunisikiliza! Nilipiga magoti chini nililia Sana siku Ile!
Nilimuomba Mirac asiniache Mimi 😰 hakujali alianza kupiga hatua taratibu kuondoka mahali pale nilipokuwepo akawa anaelekea ndani miraaaaac miraaaaac usiniache 😭😭😭 Kwa hiyo hata wewe umekuwa kama Oskar!? Nililia Kwa nguvu na Kisha nilimuuliza Mirac hivyo baada ya kupaza sauti yangu kumuita Mirac huku nikiwa nalia Mirac alisimama alifuta machozi yake then alinigeukia nilinyanyuka pale chini nikamkimbilia nilitua kifuani kwake sisi sote tulikuwa tunatokwa na machozi!
Baby simjui et😰😰 livia sikuamini najiuliza ni kwanini unanisaliti livia kwanini mbona nakupenda na mapenzi yangu yote ninakupatia why unanifanyia hivyo Livia 😰 Mirac aliongea hivyo Kisha alinitoa kifuani kwake akawa ameelekea ndani nilimfuata nyuma lakini aliingia chumbani kwake akajifungia hakutaka kabisa kuongea na Mimi nilielekea katika chumba Cha wageni nikaenda kulala huko
Nilijaribu kulazimisha usingizi lakini Wala haukuja nilikaa tu kule chumbani huku nikiwa natokwa na machozi πŸ˜₯πŸ˜₯ why meπŸ˜₯😰 cjy hata nilisinzia sangapi nilikuja shtuka asubuhi saa mbili haraka nilirauka kitandani nilielekea washing room nikajifanyia usafi Baada ya hapo nilienda kugonga chumbani Kwa Mirac nilijua huenda hasira zake zitakuwa zimepungua Ili tuweze kuongea! Nilibisha sana pale mlangoni..... Sorry madame boss hayupo amesafiri hii hapa barua kaniachia nikupatie! Alikuwa ni Neely yule Binti yangu wa kazi alisogea pale Karibu yangu akawa amenipatia barua kutoka Kwa Mirac! Aliondoka muda Gani!? Aliondoka saa 11 alfajili!
Jerome ni nani!? Kipi anachokihitaji!? Mirac kaenda wapi!? Usikose kuifuatilia simulizi hii katika sehemu inayofuata......

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...