Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji njombe Mhe. Erasto mpete
ameupokea ugeni kutoka Halamshauri ya Wilaya ya Gairo ambao umekuja kujifunza
kilimo cha Parachichi katika Halmashauri ya mji njombe .
Akizungumza Septemba 30,2024 mara baada ya kuupokea ugeni huo Mhe Mpete amewakaribishwa wageni hao ambapo
amewaomba kutembelea mashamba mbalimbali ya wakulima wakubwa na walio fanikiwa
kupitia zao hilo ili waweze kujifunza na kuyapata yale ambayo wanatarajia kupitia zao .
Kwaupande wake Mhe. Rachel Nyangasi Diwani kata ya Chigelana na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya Gairo amesema lengo la kuja kujifunza kilimo cha
parachichi Halmashauri ya Mji Njombe nikutokana na ubora ambao halmashauri ya
mji aimekuwa ikitengeneza katika zao hilo hasa kwa kuzingatia ubora ,namna ya Kaunda
mashamba ya parachichi na hatau mbalimbali za kuanzishwa kwa mashamba ya zao
hilo hadi katika masoko .
Halmashauri ya wilaya ya Gairo wamekuja na
wataalamu wa kilimo ,Biashara pamoja na Waheshimiwa
madiwani wa wilaya hiyo ambayo imekuwa ikilima mazao mablimbali hasa alizeti na
mahindi.
Na Mwandishi wako Mario Mgimba
0622467223
No comments:
Post a Comment