Monday, 28 October 2024

MPETE: AWATAKIA WANAFUNZI WOTE WA H/M/NJOMBE MTIHANI MWEMA KIDATO CHA PILI

Oktoba 27 ,2024  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Erasto Mpete aliwatakia Mtihani mwema wanafunzi wote wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Utalingolo kwa niaba ya Shule zote za Halmashauri ya Mji Njombe ambao tayari wameanza mtihani wao wa  taifa wa upimaji tarehe 28 oktoba hadi tarehe 7 Novemba 2024.


Akiwa katika shule hiyo Mhe Mpete amewaomba wanafunzi hao kufanya vema mitihani hiyo ambayo itakuwa kipimo kikubwa katika taaluma yao ya kuendelea na masomo kidato cha tatu pamoja na kuwasisitiza umakini wawapo katika vyumba vya mitihani.


Mwenyekiti alitoa Peni kwa wanafunzi wote wa kidato cha pili kwa ajili ya mitihani hiyo.



Saturday, 26 October 2024

VINCENT MGINA AWAGUSA WANAFUNZI WA KIKE SHULE YA SEKONDARI MADILU

 VINCENT MGINA AWAGUSA WANAFUNZI WA KIKE  SHULE YA SEKONDARI  MADILU.


Mtendaji wa kata ya Madilu Zaveria Mduda kwa kushirikiana na mkazi wa kata hiyo Vincent Mgina wamegawa taulo za kike kwa wanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari Madilu wanaotarajia kuanza mitihani yao ya Taifa ya kujipima  ili iwasaidie pale ambapo watakuwa katika mitihani hiyo.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi hao oktoba 26 ,2024  Zaveria Mduda  amemshukuru mdau huyo kwa kujitoa  kwa moyo wote  hasa kwakuwagusa wanafunzi hao ,jambo ambalo litaleta hamasa katika kukuza taaluma ya kata hiyo pamoja na kuwafanya wanafunzi kujisikia vizuri wakiwepo shuleni na kuweza kufanya mitihani yao vizuri.































Thursday, 17 October 2024

TAMISEMI NA VODACOM KUENDELEZA MASHIRIKIANO

 TAMISEMI NA VODACOM KUENDELEZA MASHIRIKIANO


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Ndugu. Adolf Ndunguru amekutana na wawakilishi kutoka Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mpesa Vodacom Tanzania Bw. Epimack Mbeteni ofisini kwake Jengo la Sokoine Jijini Dodoma.


Bw. Nduguru amesema Ofisi yake itaendelea kushirikiana na Vodacom kwa lengo la kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wote.


Naye Bw. Mbeteni  kutoka Vodacom ameahidi kuendeleza ushirikiano kwenye shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kuwafikia wananchi hasa wa ngazi ya chini kabisa ambako TAMISEMI inafika.


Wednesday, 16 October 2024

Njombe yafanya Vizuri Zoezi la UANDIKISHAJI WA wapiga Kura

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amesema hadi kufikia jana Oktoba 14, 2024 ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchagizi wa Serikali za Mitaa, katika mikoa 26 asilimia 45 ya Watanzania walikuwa wamekwishaandikishwa.


Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Jijini Mwanza alipokuwa akizungumza  na waandiashi wa habari kuhusu uchaguzi wa Serikaliza Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.


Ameitaja mikoa inayofanya vizuri kwenye  uandikishaji kuwa ni Tanga (54.7%), Ruvuma (46.5%), Njombe (45.1%), Songwe (44.6%) na Iringa (40.6%). 


Kwa upande wa ile ambayo bado iko chini ya wastani tarajiwa ni Katavi (23.9%), Kilimanjaro (25.1%), Geita (25.5%), Kigoma (26.1%) na Manyara (26.9℅).


Mchengerwa amewaagiza  Wakuu wa Mikoa yote Tanzania kufuatilia halmashauri ambazo uandikishaji upo chini na kutatua changamoto zilizobainika ili kwa siku zilizobaki idadi ya watu wanaojiandikisha iweze kuongezeka.


Monday, 7 October 2024

MIKATABA YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA AFYA NA ELIMU NJOMBE TC YASAINIWA

 


Oktoba 07,2024 Halmashauri ya mji Njombe Imesaini mikataba ya ujenzi wa miundombinu ya Shule na Afya na kamapuni ya Ingenuity works Limited na Hamerkop International Limited.

Akizungumza katika hafla hiyo  Mwenyekiti wa halmashauri ya mji njombe Mhe Erasto Mpete ameziomba kampuni hizo kwenda  kutekeleza miradi hiyo kwa ubora na ufanisi mkubwa  kama ilivyo tarajiwa na wananchi .

“Mhe Rais  Dkt .Samia Suluhu Hassan amekuwa akitafuta fedha kwa nguvu kubwa hivyo anatamani kuona utendaji wa kazi unakuwa kwa kiwango kikubwa na  tunatarajia mnaenda kufanya kazi kwa utaratibu na miongozo miliyopewa kwa kufanya kazi vizuri ili kuendana na thamani ya miradi hiyo,imani yangu mtafanya kazi vizuri na kwa unadhifu mzuri tofauti na mafundi wingine” Alisema Mhe Erasto mpete .

Mikataba hiyo itaenda kutekeleza Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Wikichi Kata ya Ramadhani kwa shilingi Milioni 580,Ujenzi wa Mabweni 2 shule ya sekondari Matola kwa shilingi milioni 280 na Ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje ( OPD ) Hospitali ya Kibena Shilingi milioni 965.










Friday, 4 October 2024

TOENI TAARIFA VITENDO VYA UKATILI KATIKA JAMII

 Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Njombe Petro Mahanza amewataka wazazi hukakikisha wanaripoti vitendo  vya ukatili vinavyo tokea katika jamii .



Wito huo umetolewa Oktoba 02 ,2024 Katika Mkutano wa Hadhara Kata ya Uwemba ambapo Mahanza amewatka wazazi wote wa kata hiyo kuhakikisha wanaripoti vitendo vya ukatili kutokana na baadhi ya watu kuficha watu ambao wanafanyiwa ukatili majumbani.



kwa Uapnde wake Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Njombe Fransisca Mosha  amewataka wazazi kuhakikisha wanazingatia ulaji bora unaozingatia makundi yote matano ya vyakula kwa watoto .


katika Mkutano huo Elimu ya kushiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 imetilewa ambapo wanachi wote na wakazi wa kata. hiyo wametaliwa Kushiriki zoezi Hilo.

MKENDA :RAIS AMEFANYA MAGEUZI MAKUBWA SANA SEKTA YA ELIMU LUDEWA

 Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia nchini Prof.Aldof Mkenda amezindua nyumba ya mwalimu shule sekondari Lubonde wilayani Ludewa mkoani Njombe ambayo imegharimu zaidi ya mil 97 katika ujenzi wake.

Wakati akizindua Prof Mkenda amesema serikali ya mama Samia imedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya elimu kwa kujenga na kuboresha miundombinu kote nchini na kisha kuondoka na ombi la ujenzi wa mabweni shuleni hapo.
Awali diwani wa kata ya Lubonde Edger mtitu amesema kitendo cha serikali kujenga shule ya sekondari katika kata hiyo changa kimeondoa changamoto ya watoto kufata elimu umbali mrefu na kisha kueleza kiu ya wananchi kuona shule hiyo inakuwa na mabweni ya wanafunzi wote na kuomba serikali kuona namna ya kuwasaidia huku mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga akitumia fursa hiyo kuomba walimu wa masomo ya sayansi.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Lubonde Willy Chaula amesema wametekeleza mradi wa nyumba ya walimu kwa kutumia fedha ya mradi wa kuboresha elimu wa SEQUID ambapo kiasi cha mil 100 kilitolewa kwa ajili ya ujenzi wake. 

DIDA WA WASAFI AFARIKI DUNIA


 

Thursday, 3 October 2024

APOKONYWA MALI ZOTE NA KULUDI KWA EX ...WAKE ALIA NA KUSAGA MENO

 Muigizaji maarufu wa Marekani Tyrese Gibson ameangua kilio kikali baada ya mke wake  kushinda kesi ya talaka na kuchukua mali zote za jamaa ikiwemo jumba lake na binti yao kisha mwanamke huyo kurudiana na ex wake wa zamani.


Unaambiwa Tyrese amepigwa marufuku kukanyaga kwenye nyumba hiyo mpaka aalikwe tu na amepewa ruhusa ya kumuona mwanae mara 3 tu kwa mwezi


Mke wa Tyrese amesema alikubali kuolewa na Tyrese sababu ya umaarufu tu ila hakuwa na hisia nae kimapenzi hata kidogo na wakati wote akiwa na Tyrese alikuwa akifanya mawasiliano na huyo ex wake


Anasema ex wake ndio mwanaume waliyependana kwa dhati japo hakuwa na pesa wala umaarufu ila hisia zake zote daima zilikuwa kwa njemba huyo


Unaambiwa saiv huyo jamaa anaishi nyumba ya Tyrese na mke wa Tyrese (mtalaka), mwamba anafinyia kwa ndani


Tyrese kapoteza kila kitu, wanawake mna matukio sio poa 



Jamaa amelia mno aisee 😭😭😭😭

MAHENGE :NJOMBE TC INAKILA AINA YA FURSA ZA KILIMO

 



Mkamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji njombe amewakaribisha watu wa hai kuja kutembelea halmashauri ya mnji njombe kutokana na fursa za kilimo zinazopatikani Mkoani hapo.

Amezungumza hayo oktoba 02,2024 katika ofisi za halmashauri ya mji njombe na wageni kutoka Halmashauri ya wilaya ya Hai waliokuja kutembelea Halmashauri ya mji Njombe ambapo Mkamu Mwenyekiti aliwa pongeza kwa kuja kutembelea halmashauri ya mji njombe na kwa ugeni huo ambao umekuja utaleta chachu ya kukuza uchumi kwa halmashauri hizo.













Aliongeza kwa kusema Halmashauri ya mji Njombe imepiga hatua kubwa sana katika zao la parachichi kwani maelfu ya wananjombe wanajihusha na zao la parachichi  na wanajipatia fedha nyingi kupitia zao hilo.

MEDDA :TWENDENI TUKAJIANDIKISHE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

 


Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Mji Njombe Samson Medda amewataka wananchi wote Halmashauri ya mji njombe kuhakikisha wanashiriki  na kujiandikisha kwenye Orodha ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Novemba 27,2024.

Amesema hayo oktoba 03 ,2024 kwenye kikao kazi cha uwasilishaji wa mpango kazi wa shughuli za maendeleo na kutafsiri 4R za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kata ya njombe mjini kwa mwaka 2024/2025 ambapo Medda amewaomba wakazi wote wa njombe mjini kuhakikisha wanshiriki katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa kama 4R za mhe rais zinavo tafsiri.

Aidha Medda ameupongeza uongozi wa kata ya njombe mjini kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kata ya njombe mjini kwa kutokana na miradi mbalimbali kutekelezwa kama vituo vya afya ,madarasa  na Ruzuku za kilimo kwa wakulima.

Alatanga Nyagawa Diwani wa kata ya Njombe Mjini amewaomba wananchi  wa kata hiyo kuendelea kutunza mji kwa usafi wa mazingira .






Dkt. Naiman Besta:CHANGAMOTO SASA BASI ,PELEKENI WATOTO SHULE






 Mtaalamu wa Masuala ya Jamii kutoka Benki Kuu ya Dunia  Dkt. Naiman Besta aipongeza halmashauri ya Mji Njombe kwa kutekeleza vema miradi ya kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi (BOOST) na  Miradi ya Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP

 

Akizunguma Oktoba 01,2024 akiwa katika Shule ya Msingi Mpya ya Mapinduzi kata ya Iwungilo na Shule ya Sekondari Lunyanywi  Dkt Naiman ametoa pongezi kwa wataalamu na madiwani kwa kusimamia  vema ujenzi wa shule hizo mpya.












“Kwa miradi ambayo tumeiona hapa ni ukwelikwamba kunausimaizi mzuri niombe tuendele kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan” alisema Dkt. Naiman Besta.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora wa Shule, Mwalimu Monica Mpololo, ameongoza ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa wa Njombe chini ya Mpango wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na mradi wa BOOST. Ukaguzi huo ulihusisha maafisa kutoka OR-TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na wafadhili kutoka Benki ya Dunia.

Lengo kuu la ukaguzi huu ni kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha mazingira ya utoaji elimu katika shule za msingi na sekondari nchini. Miradi inayokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari, madarasa ya awali ya mfano, miundombinu ya elimu, pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ili kuongeza ubora wa elimu nchini.



KATAMBI: SERIKALI INATAMBUA UMUHIMU WA LUGHA YA ALAMA




 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa kuwa na lugha moja ya alama ili kuwezesha mawasiliano ya watumiaji wa lugha hiyo.


“Serikali imeendelea kuimarisha matumizi ya Lugha ya Alama kwa kuchukua hatua za muda mfupi, kati na mrefu. Hatua za muda mfupi ni pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watoa huduma katika Sekta mbalimbali. Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imetoa mafunzo kwa watoa huduma za Afya, Maafisia Ustawi wa Jamii, Walimu wa Shule ya Msingi na sekondari“ amesema.


Mhe. Katambi amebainisha hayo Septemba 28, 2024 katika Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye Uwanja wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga, ambayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo “TUMIA LUGHA YA ALAMA KUTIMIZA HAKI YA LUGHA YA ALAMA.”


Aidha, amelitaka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ikamilishe mwongozo wa Wakalimani wa Lugha ya Alama ambao utachangia kukua na kuenea kwa lugha ya alama pamoja na tasnia ya ukalimani.


Vile vile, ametoa rai kwa vyombo vya habari vya kitaifa vinapotangaza matukio ya kitaifa na taarifa za habari kuhakikisha Wanakuwa na Wakalimani wa lugha ya alama, Wizara na Taasisi kuchukue hatua ya kuwapeleka Watumishi kwenda kupata mafunzo ya muda mfupi ya Lugha ya Alama.


Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Selina Mlemba ameipongeza serikali kwa kuendelea kutambua umuhimu wa lugha ya alama na hivyo kutenga siku maalumu kwa ajili ya siku hiyo Pamoja na kutenga fungu kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu.


Wednesday, 2 October 2024

WANANCHI HAI DC KUNUFAIKA NA ZAO LA PARACHICHI

 






Halmashauri ya Wilaya ya Hai imefanya ziara ya kutembelea  Halmashauri ya Mji Njombe kwa lengo la kujifunza  kilimo cha parachichi na fursa mbalimbali za kiuchumi .

Akizungumza Oktoba 02 ,2024  ulipo wasili ugeni huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Kuruthum Sadick ameishukuru na kuipongeza Halmashauri hiyo kwa kuona fursa mbalimbali  za kilimo cha parachichi katiika halmashauri ya mji njombe ambapo wanachi wengi wamekuwa wakinufaika kupitia zao hilo

“Nimefurahi sana kuona mmekuja kututembelea halmashauri yetu ,naamini hamtatoka kama mlivo kuja  na sisi pia tutajifunza vitu kutoka kwenu ambavyo vitasaidia halmashauri yetu kusonga mbele na kukua zaidi kiuchumi” Alisema Kuruthum Sadick Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe.



Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Hai Mhe.. Edmund Rutaraka
amesema  kwa fursa za kilimo hasa cha parachichi ambazo wameweza kuziona zitaenda kuimarisha uchumi wa wananchi wa hai  kutokana  fursa ambazo wameziona zitakwenda Kunyanyua uchumi wa wawana wilaya hiyo hasa katika kilimo hicho ambacho kimekonga  Nyoyo zao kwa namna wananch wa njombe wanavyo nufaika kwa maelfu ya fedha kupitia kilimo hicho


Halmashauri ya wilaya Hai imetembelea Shamba la Mkulima wa Prachichi Nemes Green Garden , Soko Kuu Njombe namna linavyo fanyakazi  vizuri na  Kiwanda cha kuchakata Parachichi kilichopo Hagafilo kata ya Njombe Mji.

Ziara ya Halmashari ya wilaya ya Hai na Njombe mji italeta mapinduzi makubwa katika uchumi wa wananchi wa halmashauri hizo kwani wataenda kuibua miradi mipya  ambayo itakuwa na tija na yenye ufanisi mkubwa pamoja kuongeza diplomasia chanya ya halmashauri hizo..








AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...