🚨 MPANZU hataweza kuichezea Simba kwa sasa kutokana na kuchelewa dirisha la usajili ambapo Wekundu hao watamuongeza kwenye dirisha dogo litakalofunguliwa Desemba mwaka huu atakapoanza kucheza mashidano yote.
Kanuni za CAF zinaruhusu mchezaji atakayetumika kwenye michuano wanayoisimamia lazima awe na leseni inayomuonyesha anacheza ligi ya nchi gani. Simba italazimika kutomtumia Mpanzu katika hatua ya makundi.

No comments:
Post a Comment