Mbunge wa Jimbo.la Njombe Mjini Mhe. Deo Mwanyika ametoa shilingi laki moja kwa Mabingwa wa Mwanyika Cup kata ya Ramadhani huki na Timu ya Itulike FC wakipewa shilingi elfu hamsini na mpira mmoja mara baada ya kushindwa kutamba mbele ya wenyeji wao Itulike FC kwa mikwaju ya penati 4_5.
Akikabidhi zawadi hiyo Septemba 29,2024 Katika Uwanja wa Itulike kwa niaba ya Mbunge Emilia Mwangeni Katibu wa Mbunge Jimbo la Njombe amesema ushirikiano unaotokana na michezo ndio chachu inayopelekea Mbunge Mwanyika kuendelea kuimarisha michezo Jimboni kwake puamoja na kuboresha miundombinu ya Michezo ambayo amekuwa akiipambania akiwa Bungeni kuhakikisha vijana wananufaika na Michezo kutokana na ajira nyingi zinazotokana na michezo.
Akiendelea kuzungumza katibu wa Mbunge Ndugu Emilia amewaomba Vijana hao kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa kuchukua fomu na kutia nia katika nafasi mbalimbali za Uongozi.
kwa Upande wake Mhe .Nikson Nganyange Diwani wakata ya Ramadhani amesema mashindano hayo yametamatishwa kwa kushuhudia mitanange huo wakukata nashoka ambapo amewaomba vijana na wananchi wa mtaa huo kushiriki katika michezo kutokana na fursa zinazopatikana kypitia Michezo.

No comments:
Post a Comment