Monday, 9 December 2024

USAFI WAFANYIKA MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA NJOMBE

 Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika Kila Disemba 9 ya mwaka Wananchi mkoani Njombe wameshiriki kufanya usafi wa mazingira na kutoa misaada kwa wagonjwa huku wito ukitolewa kwa jamii kujijengea utamaduni wa kuwa safi wakati wote.


Halmashauri ya mji wa Njombe imesherekea siku hii kwa kufanya usafi katika maeneo ya Kituo cha Afya Njombe mjini,Soko kuu na kupanda miti katika shule ya sekondari Mpechi ambapo Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Njombe mjini Nicodemus Funi anasema pia wamezindua kampeni ya usafi ya siku kumi ndani ya Kata hiyo.



Wenyeviti wapya wa serikali za mitaa ya Kata ya Njombe mjini Akiwemo Malaki Mwandila na Francis Msanga wamesema jamii inao wajibu wa kuweka mazingira sawa wakati wote huku wakitoa vifaa vya usafi katika kituo cha Afya na misaada mingine kwa wagonjwa.

Kwa niaba ya Katibu Tawala wilaya ya Njombe Ofisa Tawala wilaya Bwana Benjamin Machibya ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi Kulinda amani iliyopo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Njombe wamesema usafi unasaidia kukabiliana magonjwa ya mlipuko na ndio maana wameungana na serikali kushiriki zoezi hilo.

Serikali ya Tanzania ilielekeza maadhimisho hayo yafanyike kwa ngazi za mikoa na Wilaya kwa kufanya shughuli za kijamii ambapo mkoani Njombe yamefanyika mabonanza,Usafi pamoja na kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali.

Wednesday, 4 December 2024

NYUMBA 9 MJI MWEMA NJOMBE ZAEZULIWA NA MVUA KUBWA

 

Katibu tawala Wilaya Njombe Bi. Agatha Mhaiki ametoa pole kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mwema eneo la Msete kwa maaafa ya kuezuliwa nyumba iliyosababishwa  na mvua kubwa iliyo nyesha Disemba 03,2024.











Akizungumza Katibu tawala akiwa eneo la tukio hilo Disemba 04 ,2024 alipoongoza na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Njombe amesema serikali tayari imefanya tathimini kwa nyumba zilizo pata maafa kwa ajili ya ukamilishaji wa Nyumba hizo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Akiendelea kuzungumza na wakazi hao  Mhaiki amesema kwa niabaya ya kamati ya ulinzi na usalama wamechangia shilingi laki tatu tu(300,000)kwa ajili ya wahanga hao huku taratibu zingine za ukusanyaji zikiendelea.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete amsema taratibu za uchangiaji zitaratibiwa na ofisi ya Mtendaji wa kata na Mtaa ili kuhakikisha matumizi ya fedha ambazo watakuwa wamezitoa wadau kutoka maeneo mbalimbali ziwekwe kwenye kwenye  akaunti ya Mtaa ambayo ni  6062300658 -Mtaa wa Mji Mwema ili kuepusha changamoto katika ukusanyaji.

Jumla ya Nyumba 10 Katika Mtaa wa Mji Mwema zimeezuliwa na Mvua kubwa  iliyo nyesha Disemba 03,2024 ambayo ilisababisha maafa hayo.

 

WAFANYA BIASHARA SOKO KUU NJOMBE WAPATIWA ELIMU YA MATUMIZI YA DAWA NA VIFAA TIBA

 Wafanya Biashara wa Soko Kuu Njombe na soko la wakulima Halmashauri ya mji Njombe wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba.












Akizungumza Disemba 04,2024  Maria Sanga  Afisa Elimu kwa Umma  kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyada za Juu Kusini na wafanyabiashara hao kuhakikisha wanatumia dawa kwa usahihi kama mtaalamu anavo elekeza dawa hizo. 

“Kumekuwepo na wimbi la wananchi  kutumia dawa pasipo vipimo vya daktari, kutomaliza dawa kwa muda sahihihi na wengine kutumia dawa za binadamu kwenye mifugo  niwaombe mkipata changamoto yoyote ya afya na daktari akakwambia tumia dawa hizi kwa muda wa siku kadhaa tumia muda huo kama ulivyo elekezwa usipofanya hivyo unapelekea usugu wa dawa katika mwili wako na kupelekea dawa hiyo kutofanya kazi  katika mwili wako ” Alisema Maria Sanga Kutoka TMDA

Akiendelea Kuzungumza Maria amewataka Vijana na Mabinti ambao wamekuwa wakitumia dawa za nguvu za kiume na Dawa za kuua  Mbegu za kiume maarufu (P2) zisitumike kilasiku jambo ambalo linaharibu afya zao kutokana namatumizi mabaya ya dawa hizo kinyume na makusudio yake kwa wananchi hasa kwa ambao wamekutana na changamoto .

“Watu wamekuwa wakitumia P2 kila wakifanyapo tendo la Ndoa lakini kitaalamu inatakiwa zitumike mara 2 kwa mwaka na sio kila wakimaliza tendo la ndoa na kwa wanaume dawa za nguvu za kiume zipo kwa wale ambao wanachangamoto za maumbile yao ya mfumo wa uzazi ,sio kwa watu mbao wazima mnajiua wenyewe vijana achene kuwakomoa mabinti mkiamini dawa za nguvu za kiume zinawaridhisha wanawake hapana!!!!. ” Alisema Maria Sanga Kutoka TMDA.


TMDA YAWAFIKIA WAKULIMA WA PARACHICHI NJOMBE

 










Wakulima na Wadau wa Parachichi Halmashauri ya mji Njombe watakiwa kutumia dawa na vifaa tiba kwa usahihi kama matumizi yanavowataka na sio vinginevyo.

Wito huo umetolewa Disemba 04,2024 na Maria Sanga  Afisa Elimu kwa Umma  kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyada za Juu Kusini ambapo aliwaomba wakulima na wadau hao wahakikishe wanatumia dawa hizo kama inavyo takiwa kwa mjibu wa mtaalamu husika ambaye anampa dawa hizo jambo ambalo kwa baadhi ya watu wanapata usugu wa dawa kutokana na kutumia dawa kwakutozingatia vipimo na masharti ya daktari.

“Kumekuwepo na wimbi la wananchi  kutumia dawa pasipo vipimo vya daktari, kutomaliza dawa kwa muda sahihihi na wengine kutumia dawa za binadamu kwenye mifugo  niwaombe mkipata changamoto yoyote ya afya na daktari akakwambia tumia dawa hizi kwa muda wa siku kadhaa tumia muda huo kama ulivyo elekezwa usipofanya hivyo unapelekea usugu wa dawa katika mwili wako na kupelekea dawa hiyo kutofanya kazi  katika mwili wako ” Alisema Maria Sanga Kutoka TMDA

Naye kwa Upande wake Adam Sorota Mkaguzi wa dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyada za Juu Kusini amewataka wananchi ambao wata kutana na  changamoto watoe taarifa katika kituo husika walicho pata dawa hiyo au wawasiliane na Mamlaka husika kwa mawasiliano ya kupiga namba ya simu bila malipo ya 0800 110 084.

 

Monday, 2 December 2024

ELIMU YA LISHE YATOLEWA UKUMBINI

AFISA Lishe Mkoa Njombe Betha Nyigu ametumia fursa ya kutoa elimu ya Lishe kwa wananchi walio hudhuria  sherehe ya harusi ya Afisa Lishe ajira Mpya (Damiana Danda)Njombe TC. 

Katika hafla hiyo aliweza kuwaomba wanachi wote wamkoa njombe kuzingatia elimu lishe,kula makundi yote ya vyakula na kuzingatia mlo kamili  kwa mtoto kutokana na ongezeko la udumavu kwa mkoa njombe.

Hafla hiyo pia ilihudhiriwa na maafisa lishe wa Halmashauri zote za mkoa Njombe .

Kujazatumbo sio Lishe 



#Lishe ya Mwanao, Mafanikio yake#๐Ÿ‘†๐Ÿฝ๐Ÿ‘†๐Ÿฝ๐Ÿ‘†๐ŸฝTulifikisha ujumbe kwa watu zaidi ya 1000#Kujaza tumbo si Lishe, Jali unachomlisha #

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...