Thursday, 18 September 2025

MHE. ANTHONY MTAKA AKUTANA NA VIONGOZI WA DL GROUP NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA NJOMBE

 

MHE. ANTHONY MTAKA AKUTANA NA VIONGOZI WA DL GROUP NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA NJOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya DL Group, Ndugu Dr. David Langat, pamoja na viongozi wa wafanyabiashara kutoka mkoa wa Njombe.

Katika kikao hicho walihudhuriwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali za mkoa, pamoja na vikundi vya uwakilishi kutoka kwa wanawake.









Kikao Hicho Kilijikita  katika kujadili fursa za uwekezaji katika viwanda, na namna ambavyo sekta hii itakavyoinua uchumi wa wananchi wa Njombe. Fursa za uwekezaji zilijikita katika zao la parachichi, chai, na viazi, ambapo kupitia uwekezaji katika viwanda vya usindikaji, kuna matumaini ya kuongeza mnyororo wa dhamani wa mazao haya na kuleta manufaa kwa wakulima na wajasiriamali wa eneo hili.

Mhe. Mtaka alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na sekta binafsi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Njombe, huku akitaja kuwa uwekezaji huu utasaidia kuongeza ajira, kuboresha miundombinu, na kukuza sekta ya kilimo. Wadau walieleza matumaini yao kwamba hatua hizi zitakuza uchumi wa mkoa na kuboresha hali ya maisha ya wakazi wake.

Thursday, 11 September 2025

Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Njombe TC Wapatiwa Mafunzo ya Lishe Kupunguza Udumavu

 Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Njombe TC Wapatiwa Mafunzo ya Lishe Kupunguza Udumavu

Njombe, Septemba 10, 2025 – Wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa mafunzo maalum ya utekelezaji wa afua za lishe, yakiwa na lengo la kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto na vijana balehe katika mkoa huo.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Catholic Relief Services (CRS) kupitia mradi wa Lishe ya Mwanao unaodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Lishe wa Mkoa wa Njombe, Bi. Bertha Nyingu, alisema ni muhimu wahudumu hao kuzingatia matumizi ya virutubisho kwa watoto na vijana wanaowahudumia ili kuhakikisha afya bora na kupunguza athari za lishe duni.

 “Tunasisitiza matumizi ya virutubisho kwa watoto na makundi ya balehe kwa sababu wao ndio kundi linalohitaji uangalizi wa karibu. Tukitekeleza afua hizi ipasavyo, tutapiga hatua kubwa kupunguza udumavu mkoani Njombe,” alisema Bi. Nyingu.

Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo walisema yamewajengea uwezo wa namna bora ya kutoa elimu ya lishe na huduma rafiki kwa jamii. Waliahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa vitendo ili kuboresha afya za watoto na vijana katika maeneo wanayoyahudumia.









Njombe ni miongoni mwa mikoa yenye viwango vya juu vya udumavu nchini, hivyo juhudi za kuimarisha lishe zinaendelea kupewa kipaumbele na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.


AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...