Wednesday, 26 November 2025

MAAFISA UGANI NJOMBE MJI WAPATA MAFUNZO KUHUSU MRADI WA YEFFA

 

 Novemba 26, 2025 Maafisa ugani  Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi  Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa mafunzo na  Mradi wa YEFFA kuhusu namna watakavyo tekeleza mradi  unaolenga  shughuli za kilimo kwa vijana wa eneo hilo.









Akizungumza wakati akitoa mafunzo hayokatika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Luqmaan Kimbute  kutoka  Shirika la Rikolto amesema mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa na ujuzi wa wataalamu wa kilimo kuhusu utekelezaji wa mradi wa Ujasiriamali wa Vijana na Mustakabali wa Chakula na Kilimo (YEFFA) ambao utaenda kuwasaidia vijana kujikwamua na maisha na kuongeza kipato katika maisha yao kutokana na wimbi la vijana wengi kutokuwa na ajira 


AKiendelea kuzungumza Mtaalamu huyo bwana Luqmaan amesema  mradi huo utatekelezwa kwa  miaka mitatu  ambapo utapanua fursa za ajira kwa vijana katika mnyororo wa thamani wa zao la hilo.


Kupitia ushirikiano kati ya Rikolto, Serikali, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima (hasa wanawake na vijana), vyama vya wakulima, taasisi za kifedha, watafiti na wanunuzi

wa shirika hilo linaendelea kuchangia mageuzi chanya katika kilimo na mifumo ya chakula. 


Mafunzo haya yanatarajiwa kuimarisha ufanisi wa watekelezaji wa mradi na kuleta matokeo chanya kwa jamii ya Njombe na taifa kwa ujumla.

Friday, 7 November 2025

Meneja wa Soko Kuu Njombe Aungana na Wafanyabiashara Kufanya Usafi

 Meneja wa Soko Kuu la Njombe, Ndugu Enosy Lupimo, leo tarehe 07 Novemba 2025, ameungana na wafanyabiashara wa soko hilo katika zoezi la kufanya usafi lililofanyika katika eneo la Soko Kuu Njombe. Zoezi hilo limehusisha kusafisha njia kuu za soko, mifereji ya maji machafu pamoja na maeneo ya dampo.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Ndugu Lupimo amesema kuwa lengo la usafi huo ni kuhakikisha soko linabaki katika hali ya usafi na usalama wa kiafya kwa wafanyabiashara pamoja na wateja wanaofika kununua bidhaa mbalimbali.






 “Usafi ni wajibu wa kila mmoja wetu. Tunaposhirikiana, tunaleta mazingira bora ya biashara na afya njema kwa jamii,” amesema Meneja huyo.

Aidha, amewasihi wafanyabiashara kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara ili kulifanya soko hilo kuwa mfano wa kuigwa katika Mkoa wa Njombe.

Wafanyabiashara waliopata fursa ya kushiriki wamepongeza uongozi wa soko kwa kuonyesha mfano wa vitendo na kuahidi kuendeleza

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...