Sunday, 29 June 2025

NKOMBE ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA NJOMBE MJINI

 Mkurugenzi wa Duka kubwa la simu na vifaa vya simu Njombe Mjini (Msukuma phones & Accessories) Bwana Motuli Nkombe mapema leo June 29, 2025 amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Njombe mjini

Mbali na kujishughulisha na ujasiliamali Motuli ni pia nj Daktari kitaaluma akiwa na Shahada ya kwanza.

NJOMBE: Mwanahabari Prosper Mfugale Ajitosa Kugombea Udiwani Kata ya Ihanga Kupitia CCM

 NJOMBE: Mwanahabari Prosper Mfugale Ajitosa Kugombea Udiwani Kata ya Ihanga Kupitia CCM


Juni 29, 2025 Mwandishi wa habari wa vituo vya Tumaini TV na Njombe TV, Prosper Mfugale, amejiunga rasmi katika ulingo wa siasa baada ya kuchukua fomu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya udiwani wa Kata ya Ihanga, iliyopo katika Halmashauri ya Mji Njombe.







Mfugale, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mstari wa mbele katika kuripoti masuala ya kijamii na maendeleo mkoani Njombe, amesema uamuzi wake wa kuingia kwenye siasa umetokana na dhamira ya dhati ya kutumia maarifa na uzoefu wake kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wa Ihanga.


 "Nimekuwa karibu na wananchi kwa miaka mingi kupitia kazi yangu ya uandishi wa habari. Najua changamoto zao na ninayo nia ya dhati ya kuzitatua kwa kushirikiana nao," amesema Mfugale mara baada ya kuchukua fomu.

Hatua yake imeibua hisia tofauti miongoni mwa wakazi wa kata hiyo, ambapo wengi wamepongeza uamuzi huo, wakimtaja kama kijana mwenye maono, anayeielewa jamii na anayestahili nafasi ya uongozi kwa sababu ya ukaribu wake na wananchi.


Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM unaendelea kote nchini, huku ukitarajiwa kuibua majina mapya ya watumishi wa umma, wanahabari, na wanajamii wenye dhamira ya kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao.

Nestory Mahenge Achukua Fomu ya Kugombea Tena Udiwani Kupitia CCM

 Nestory Mahenge Achukua Fomu ya Kugombea Tena Udiwani Kupitia CCM



Njombe, Juni 2025 – Aliyewahi kuwa diwani wa Kata ya Mji Mwema, Halmashauri ya Mji wa Njombe, Bw. Nestory Mahenge, amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea tena nafasi ya udiwani katika kata hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.


Hatua hiyo imekuja wakati mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ukiendelea katika maeneo yote nchini. Bw. Mahenge ni miongoni mwa viongozi waliowahi kushika nyadhifa za kiutendaji na kuacha kumbukumbu ya uongozi unaotajwa kuwa wa karibu na wananchi.


Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Mahenge alieleza dhamira yake ya kurejea kwenye nafasi hiyo ili kuendeleza miradi ya maendeleo aliyoianzisha awali, pamoja na kusimamia masuala ya kijamii na kiuchumi yanayoikabili kata hiyo.


> "Nimerudi tena kwa moyo wa kujitoa kuwatumikia wananchi wa Mji Mwema, tukishirikiana kwa karibu kuhakikisha changamoto zinazotukabili zinapatiwa suluhisho la kudumu," alisema Mahenge.

Kikundi cha Lunyanywi Fish Farm chashiriki kikamilifu kusikiliza kero za wananchi kwa siku nne mfululizo

 Kikundi cha Lunyanywi Fish Farm chashiriki kikamilifu kusikiliza kero za wananchi kwa siku nne mfululizo



Kikundi cha Lunyanywi Fish Farm kimekuwa miongoni mwa taasisi na vikundi vilivyoshiriki kikamilifu katika zoezi la kusikiliza kero za wananchi lililoratibiwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe. Zoezi hilo limefanyika kwa muda wa siku nne mfululizo katika eneo la stendi ya zamani mjini Njombe.

Lengo kuu la zoezi hilo ni kuwapa wananchi jukwaa la wazi kueleza changamoto, malalamiko na mapendekezo yao kuhusu huduma mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kiutawala, huku taasisi na mashirika mbalimbali yakishiriki kusikiliza na kutoa mrejesho wa haraka.

Kikundi cha Lunyanywi Fish Farm kimeeleza kuwa kushiriki kwake katika zoezi hilo ni sehemu ya wajibu wao wa kijamii  na nia ya dhati ya kushirikiana na serikali na wananchi kuboresha maisha ya jamii inayowazunguka kuhusu ufugaji wa samaki .

Wawakilishi wa kikundi hicho kinachoongozwa na Mussa Lupenza ameelezea kuwa wamepokea maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi kuhusu umuhimu wa chakula cha samaki, na changamoto zinazowakabili wafugaji wa samaki wadogo wadogo katika mji wa Njombe.


“Tumejifunza mengi kutoka kwa wananchi. Wameeleza kiu yao ya kupata mafunzo ya ufugaji bora wa samaki, upatikanaji wa vifaranga na masoko ya uhakika. Sisi kama Lunyanywi Fish Farm tupo tayari kushirikiana nao katika kutatua changamoto hizi.” Alisema Mussa Lupenza

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya kilimo ,mifugo ma Uvuvi Thadei Luoga   kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, alilipongeza kundi hilo kwa ushiriki wao na kuwataka wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano huo wa kuwafikia wananchi moja kwa moja.

Zoezi hilo la kusikiliza kero limeonekana kuleta matumaini kwa wakazi wa Njombe, ambao wameeleza kufurahishwa na usikivu na mwitikio wa taasisi na vikundi vinavyoshiriki.



Adriano Tunduru (JANGALA) Achukua Fomu ya Kugombea Udiwani Kata ya Mji Mwema – Makambako

 Adriano Tunduru (JANGALA) Awasilisha Fomu ya Kugombea Udiwani Kata ya Mji Mwema – Makambako




Mjumbe wa Kamati ya Siasa na kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Adriano Tunduru, maarufu kwa jina la JANGALA, ameonesha nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi kwa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Mji Mwema, Halmashauri ya Mji wa Makambako.


Hatua hii inaonesha dhamira yake ya kuendelea kuwa chombo cha kuwaletea maendeleo wananchi wa Mji Mwema kupitia ushawishi, uzoefu na mchango wake katika siasa na shughuli za kijamii. Tunduru ni mmoja wa viongozi waliowahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama na anayefahamika kwa uzalendo, uwazi na kusimamia maendeleo ya kweli kwa wananchi.


Wananchi na wanachama wa CCM wamepokea kwa furaha hatua hii ya Jangala, wakionesha matumaini makubwa kuwa atakuwa chaguo sahihi kwa maendeleo ya Kata hiyo, endapo atateuliwa na chama.


Thursday, 26 June 2025

Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Kutoka Njombe TC na Njombe DC Wapatiwa Mafunzo ya Kuboresha Lishe Katika Jamii

 


Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Wapatiwa Mafunzo Kuboresha Lishe Katika Jamii za Njombe

Njombe – Jumla ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii 31 kutoka vijiji mbalimbali vya Halmashauri ya Mji Njombe na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wamepatiwa mafunzo muhimu yanayolenga kuboresha huduma za lishe katika jamii wanazozihudumia. Mafunzo haya yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la COUNSENUTH kupitia mradi wa LISHE YA MWANAO, ukishirikiana na Catholic Relief Services (CRS).

Katika mafunzo hayo, wahudumu wamefunzwa jinsi ya kujaza taarifa katika vitabu vya rufaa, vitabu vya malezi lishe, na vitabu vya jiko darasa. Pia walijifunza namna ya kusajili walengwa wa huduma za lishe kupitia Mfumo wa USSD, hatua itakayowawezesha kupokea jumbe za lishe moja kwa moja kwenye simu zao. Mfumo huu unalenga kuwawezesha wahudumu kuwafikia wanajamii kwa ufanisi zaidi kwa njia ya teknolojia rahisi na ya kisasa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Vivian Lilandeka, Afisa Mradi kutoka COUNSENUTH, alisisitiza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha wahudumu wa afya wana uelewa wa kutosha kuhusu uingizaji wa taarifa sahihi na matumizi ya mifumo ya kisasa ya mawasiliano. Alibainisha kuwa mafunzo haya yanaendeshwa chini ya kaulimbiu ya mradi huo isemayo: “Kujaza tumbo siyo lishe, jali unachomlisha.”

Kwa upande wake, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji Njombe, Damina Danda, aliwataka wahudumu hao kuhakikisha wanatoa elimu ya lishe kwa kila mama mjamzito pamoja na vijana balehe, hasa wale wanaotarajia kuanzisha familia. Alieleza kuwa makundi haya yanahitaji lishe bora kwa kiwango kikubwa ili kuepuka matatizo ya afya na udumavu.

Mradi wa LISHE YA MWANAO unalenga kusaidia jitihada za kupunguza kiwango cha udumavu mkoani Njombe, ambao kwa miaka mingi umekuwa miongoni mwa mikoa yenye viwango vya juu vya utapiamlo nchini. Kupitia mafunzo haya, wahudumu wa afya watakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha jamii inapata elimu ya lishe na huduma zinazostahili, huku lengo likiwa ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030, udumavu katika mkoa wa Njombe unakuwa historia.

Mafunzo haya ni hatua muhimu kuelekea kujenga jamii yenye afya bora na uelewa wa lishe unaotakiwa kwa maendeleo endelevu ya mkoa wa Njombe na taifa kwa ujumla.

Sunday, 22 June 2025

Dawati la Huduma za Ustawi wa Jamii lazinduliwa Stendi Kuu Njombe

 



Shirika la Railway Children Africa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Njombe limezindua rasmi Dawati la Huduma za Ustawi wa Jamii katika Stendi Kuu ya Mabasi Njombe, likiwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha usalama na ustawi wa watoto na makundi mengine yaliyo hatarini unazingatiwa.

Akizungumza juni 20,2025  katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Gabriel Kulaba, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa stendi kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa huduma muhimu sasa zimesogezwa karibu nao.

Akielezea umuhimu wa dawati hilo, Subira Mshana Mwakilishi wa shirika la Railway Children Africa wamesisitiza kuwa hii ni hatua ya utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Madawati ya Huduma za Ustawi wa Jamii katika Vituo vya Usafiri.

“Tunataka kuhakikisha kila mtoto na mwananchi aliyopo katika maeneo ya stendi anapata huduma stahiki kwa wakati, bila kujali mazingira aliyopo pasipokufanyiwa unyanyasaji ,” Alisema Subira Mshana.

Mradi huo umefadhiliwa na shirika la Railway Children Africa kwa lengo la kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika maeneo ya umma, hasa vituo vya usafiri kama stendi Kupitia dawati hilo, jamii itapata huduma za ushauri, ulinzi, na msaada wa haraka kwa watoto walioko katika mazingira hatarishi.


Dawati hilo pia litakuwa na Kamati Maalum itakayofuatilia kwa karibu matukio ya ukatili, kutoa taarifa, na kuratibu misaada ya dharura kwa watoto walioko hatarini. Aidha, jamii imetakiwa kushiriki kikamilifu kwa kutoa taarifa na kusaidia juhudi hizi kwa moyo wa kujitolea.

shirika la Railway Children Africa limeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa stendi ya Njombe inakuwa mfano wa kuigwa kama eneo salama na rafiki kwa watoto na makundi mengine maalum.

Thursday, 19 June 2025

KATIBU WA CCM WILAYA YA NJOMBE AZINDUA JENGO JIPYA LA OFISI KATA YA LUGENGE

 

KATIBU WA CCM WILAYA YA NJOMBE AZINDUA JENGO JIPYA LA OFISI KATA YA LUGENGE

Njombe, Tanzania –

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe, Ndugu Mariam Kireti, amefanya ziara maalum katika Kata ya Lugenge ambapo alizindua rasmi jengo jipya la ofisi ya CCM katika kata hiyo. Tukio hilo muhimu limehudhuriwa na viongozi wa chama, madiwani wa Halmashauri ya Mji Njombe, wanachama wa CCM, pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Lugenge.
















Akizungumza juni 19 ,2025 katika hafla hiyo, Ndugu Mariam Kireti aliwapongeza viongozi na wanachama wa CCM Kata ya Lugenge kwa juhudi na mshikamano walioonesha katika kuhakikisha mradi huo wa ujenzi unakamilika kwa mafanikio makubwa. Alieleza kuwa jengo hilo litakuwa chachu ya maendeleo kwa kuongeza ufanisi katika shughuli za chama, kuimarisha utendaji na kuweka mazingira bora ya kutoa huduma kwa wanachama na wananchi.

Katika hotuba yake, Katibu huyo aliwahimiza wakazi wa Lugenge na wanachama wa CCM kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba. Alisema kuwa mafanikio ya maendeleo nchini yanatokana na uongozi thabiti wa Rais Samia, hivyo ni muhimu wananchi wote kuendeleza mshikamano na imani kwa serikali ya awamu ya sita.

Katika kilele cha hafla hiyo, uongozi wa CCM Kata ya Lugenge ulimkabidhi zawadi maalum Ndugu Mariam Kireti kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya chama wilayani Njombe na kwa heshima ya uwepo wake katika tukio hilo.

Naye Diwani wa Kata ya Lugenge, Mheshimiwa Filoteusi Mligo, alitumia jukwaa hilo kuwapongeza wakazi wa Lugenge kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kata yao. Alisema ushirikiano huo wa karibu kati ya wananchi na viongozi umewezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa ofisi hiyo ya kisasa ya chama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lugenge alieleza kuwa jengo hilo limejengwa kwa ushirikiano wa wanachama, viongozi wa chama, na wadau wa maendeleo, na kuahidi kuwa litatumika kikamilifu katika kusimamia utekelezaji wa sera na Ilani ya CCM kwa manufaa ya jamii.

Hafla hiyo ilipambwa na burudani kutoka kwa vikundi vya ngoma za asili, nyimbo za kizalendo, na chakula cha pamoja, huku wakazi wa Lugenge wakionesha furaha yao na kujivunia maendeleo yanayoletwa na chama chao.


AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...