Oskar alibakia kule chini huku akiwa ananitumbulia macho machozi yalimjaa katika macho yake na yalianza kumdondoka liviaaaaa aliniita huku akiwa ananyuka kunifuata! Mirac aliniweka nyuma ya mgongo wake hakutaka kabisa Oskar anisogelee! Broo huyu ni mwanamke wangu na tayari ana Mtoto wangu Oskar alimwelezea Mirac lakini Kwa bahati mbaya Mirac hakumuelewa Kwa sababu alikuwa hasikii kiswahili
Mirac na marafiki zake walikaa huku Tanzania Kwa siku Tano baada ya Hapo walirudi uturuki Mimi nilibakia Tanzania kusubilia ndoa ya Daddy & Mommy! Baada ya ndoa ya wazazi wangu niliondoka kurudi chuoni Emre nilimuacha Kwa Mom Kwa sababu hawakutaka kabisa Mimi niondoke naye! Sikurudi Tena kuishi hostel niliendelea kukaa Kwa Mirac maisha yaliendelea Mirac alinivisha Pete ya uchumba aliwatuma wazazi wake wakaenda nyumbani kwetu Tanzania Kwa ajiri ya kuniposa! Ananipenda 
Mimi ndo usiulize 
baada ya wazazi wa Mirac kwenda nyumbani kwetu kuonana na wazazi wangu Daddy and Mommy walinipigia wakaniuliza kama kweli Niko tayari kuolewa niliwaambia tu wapokee posa Kwa sababu tayari Mirac amekwisha nivisha Pete ya uchumba! Wazazi wangu walipokea posa baada ya Mimi kuwa nimewaruhusu wao kufanya hivyo! Penzi letu Mimi na Mirac lilizidi kunoga Kila siku
Siku Moja ilikuwa ni usiku nilikuwa zangu jikoni na Mirac tunaandaa chakula mara simu yangu iliita ilikuwa ni namba ngeni nilipokea baada ya kuipokea ilisikika sauti ya kiume ni ya mtu ambaye simfahamu kabisa!
Alijitambulisha ya kwamba yeye ni Jerome na alikuwa anahitaji kuonana na Mimi nilijaribu kumhoji namba yangu katoa wapi aliniambia ya kwamba Kuna rafiki yangu mmoja ndo amempatia namba! Mmhhh nilionyesha msikitiko.... Baby mbona uko hivyo ulikuwa unaongea na nani kwani!? Aliniuliza Mirac! Baby Kuna mtu kanipigia kajitambulisha kuwa yeye ni Jerome lakini simfahamu na anataka niende nikaonane naye! Hebu nipatie namba yake! Mirac aliniomba nimpatie namba ya huyo Jamaa nilimpatia namba akawa amempigia!
""Hello aliongea Mirac ""
""Hello nani!?""
""Mirac Mme mtarajiwa wa livia umempigia mwanamke wangu mda si mrefu ukiwa unahitaji kuonana naye kwani wewe ni nani!?""
""Ahahahahahaaaa huyo ni demu wangu wa mda mrefu sana Jana nilikuwa Naye na hata leo nimemkumbuka nikaona nimpigie akiweza aje tujikumbushie mapenzi kama aliyonipatia Jana broo tafuta pesa mwanamke anatulizwa na pesa na siyo hizo kelele unazonipigia unajinadi kuwa huyo ni demu wako mbona akiwa na Mimi Huwa anakataa ya kwamba Hana mwanaume tafuta pesa boys wewe! Demu ni chaote huyo wahuni tunajimegea tu kisela hata Jana Mimi mbona nilikuwa Naye tumejiachia sana Jana na alinipatia Penzi 
aliongea yule Mr Jerome tena Kwa kebehi baada ya Mirac kuambiwa hivyo alianza kuichanganua Ile kauli ya kwamba mbona hata Jana Mimi nilikuwa naye' livia Jana uliniaga kuwa unatoka so ulienda kuonana na Jerome!? Aliniuliza Mirac! nilitoka kwenda shopping sikwenda kuonana na yeyote! Livia unanicheat!? No baby unajua kabisa Mimi siwezi kufanya hivyo
vile naogopa kuachwa Tena Kwa mara nyingine nilijikuta machozi yameshaanza kunitoka nilimpigia Mirac magoti nikamwambia darling niamini siwezi kufanya hivyo kwako nakupenda et!
Mirac aliniangalia Kwa hasira aliunyanyua mkono wake akataka kunitia konzi lakini alijizuia baada ya Hapo aliondoka akaniacha pale jikoni peke yangu aliingia chumbani akavaa koti la kujikinga na baridi baada ya Hapo alielekea parking akapanda kwenye gari lake akawa ameondoka! Nilizima majiko haraka nikawa nimechukua gari ili niweze kumfuatilia Mirac nilimfuata nyuma nyuma Hadi katika lodge Fulani alishuka pale akawa ameagiza kinywaji kikali na kuanza kunywa bila kupumzika nilifika pale nikampigia magoti nilimwambia Baby tafadhari nakuomba uniamini nakupenda wewe peke Yako! Livia hata Kwa Yale yote niliyoyafanya kwako hauridhiki kipi ambacho sijakufanyia livia!? Kwanini unanisaliti livia
alinisogelea akaninyanyua pale chini Kwa hasira aliniambia Livia nakuchukia
Mirac aliongea Kwa hasira huku machozi yakiwa yanamtoka nililegea nafsi na roho nilitamani tu nife Kwa sababu kitu kuachwa sikutaka Tena kinitokee katika maisha yangu Mirac baada ya kuniambia vile alinisukuma nikadondokea chini hakujali Kabisa
alilipia kile kinywaji alichokuwa kaishakiagiza baada ya Hapo alisepa akaniacha pale chini niliendelea kukaa na kulilia pale chini nilimuuliza Mungu kwani Mimi Sina bahati ya kupendwa milele mbona Kila anayekuja kwenye maisha yangu nikishakoleza tu upendo kwake ananiacha bila kujali ni maumivu kiasi Gani nitakayoyapata! Mwenyezi Mungu fanya kitu naomba unirudishie Mirac wangu
siko tayari kutengana naye!
nililia walinzi wa kule lodge walikuja wakanitoa pale chini wakanipeleka kwenye gari Yangu! Nilikaa huko ndani ya gari huku nikiwa najiuliza nirudi Kwa Mirac au nielekee wapi 
hata Ile gari niliyokuwa nayo usiku ule ni gari yake aliyonizawadiaga siku ya birthday yangu je niirudishe hii gari nyumbani kwake usiku huu lakini ananichukia sitakiwi kuonekana katika macho yake
nikiwa pale ndani ya gari langu simu yangu iliita nilivyoangalia anayepiga alikuwa ni Jerome nilipokea Kwa hasira na kuanza kumtirilishia matusi makali Sana! Jerome alicheka sana Aliniambia livia mpenzi kwenye gari ya bwana wako Kuna kitu nimekiweka Nina Imani ni lazima tu atakupatia! Kitu
kwenye gari ya Mirac!? Nilikata Ile simu haraka nikaondoka pale lodge kuelekea nyumbani kule Kwa Mirac! Nilifika getini nikabonyeza kengere kijana wa getini alikuja haraka kunifungulia niliingiza gari ndani nikaiweka parking baada ya Hapo nilitelemka kule ndani ya gari lakini kabla sijapiga hatua Mirac alinifuata pale!
Mirac alifika akanitupia barua usoni kwangu alinikamata Kwa hasira akaniambia livia Kwa hiyo hata ndani ya gari langu unathubutu kuacha uchafu kama huu!? zilikuwa ni barua mbili Moja ilionekana kutoka Kwa Jerome na nyingine ilionekana ni kama Mimi ndo niliyeandika Tena ilikuwa ni mwandiko kama wangu kabisa barua zile mbili ilionekana ni kama Mimi nilipokea barua kutoka Kwa Jerome Kisha namimi nikamwandikia barua ambayo Bado ilikuwa haijatumwa kwake! Nilihisi kupagawa baada ya kuzisoma zile barua nilikumbuka Jana ni kweli nilitoka na hiyo gari ya Mirac lakini mbona sikumpatia mtu yoyote lift ni nani huyo aliyeweza kuingiza barua kama hizi kwenye gari ya Mirac inamaana huu mchezo nilianza kuchezewa tangu Jana bila kujua chochote 
!
Mirac tafadhari nakuomba unipe muda tuongee et kweli nakuapia simfahamu huyu mtu na hata hizi barua Mimi sijaziandika et! Mirac alicheka Kwa uchungu aliyafuta machozi yake Kisha akaniuliza Livia kwani ni kipi ulichokihitaji nikashindwa kukutimizia!? Nilikupatia Kila kitu Livia
lakini unathubutu kuandika barua kumwandikia mwanaume mwingine barua kama hiyo Kwa hiyo hunipendi eh
!? Nakupenda Mirac simfahamu Jerome simfahamu nakuapia babangu tafadhari nakuomba uchukue muda ulichunguze hili Mimi nahisi tu Kuna mtu ambaye ananifanyia mchezo mbaya nakuomba usiniache Mirac wangu usiniache nakupenda naomba usije ukaniacha et

Livia chukua Kila kilicho chako kwenye hii nyumba uondoke nakuchukiaaaa
sipendi usaliti katika maisha yangu! nilijaribu kujielezea lakini Mirac alikuwa na hasira sana hakutaka kabisa kunisikiliza! Nilipiga magoti chini nililia Sana siku Ile!
Nilimuomba Mirac asiniache Mimi
hakujali alianza kupiga hatua taratibu kuondoka mahali pale nilipokuwepo akawa anaelekea ndani miraaaaac miraaaaac usiniache 

Kwa hiyo hata wewe umekuwa kama Oskar!? Nililia Kwa nguvu na Kisha nilimuuliza Mirac hivyo baada ya kupaza sauti yangu kumuita Mirac huku nikiwa nalia Mirac alisimama alifuta machozi yake then alinigeukia nilinyanyuka pale chini nikamkimbilia nilitua kifuani kwake sisi sote tulikuwa tunatokwa na machozi!
Baby simjui et
livia sikuamini najiuliza ni kwanini unanisaliti livia kwanini mbona nakupenda na mapenzi yangu yote ninakupatia why unanifanyia hivyo Livia
Mirac aliongea hivyo Kisha alinitoa kifuani kwake akawa ameelekea ndani nilimfuata nyuma lakini aliingia chumbani kwake akajifungia hakutaka kabisa kuongea na Mimi nilielekea katika chumba Cha wageni nikaenda kulala huko
Nilijaribu kulazimisha usingizi lakini Wala haukuja nilikaa tu kule chumbani huku nikiwa natokwa na machozi 
why me
cjy hata nilisinzia sangapi nilikuja shtuka asubuhi saa mbili haraka nilirauka kitandani nilielekea washing room nikajifanyia usafi Baada ya hapo nilienda kugonga chumbani Kwa Mirac nilijua huenda hasira zake zitakuwa zimepungua Ili tuweze kuongea! Nilibisha sana pale mlangoni..... Sorry madame boss hayupo amesafiri hii hapa barua kaniachia nikupatie! Alikuwa ni Neely yule Binti yangu wa kazi alisogea pale Karibu yangu akawa amenipatia barua kutoka Kwa Mirac! Aliondoka muda Gani!? Aliondoka saa 11 alfajili!
Jerome ni nani!? Kipi anachokihitaji!? Mirac kaenda wapi!? Usikose kuifuatilia simulizi hii katika sehemu inayofuata......

No comments:
Post a Comment