Oktoba 27 ,2024 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Erasto Mpete aliwatakia Mtihani mwema wanafunzi wote wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Utalingolo kwa niaba ya Shule zote za Halmashauri ya Mji Njombe ambao tayari wameanza mtihani wao wa taifa wa upimaji tarehe 28 oktoba hadi tarehe 7 Novemba 2024.
Akiwa katika shule hiyo Mhe Mpete amewaomba wanafunzi hao kufanya vema mitihani hiyo ambayo itakuwa kipimo kikubwa katika taaluma yao ya kuendelea na masomo kidato cha tatu pamoja na kuwasisitiza umakini wawapo katika vyumba vya mitihani.
Mwenyekiti alitoa Peni kwa wanafunzi wote wa kidato cha pili kwa ajili ya mitihani hiyo.

No comments:
Post a Comment