Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amesema hadi kufikia jana Oktoba 14, 2024 ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchagizi wa Serikali za Mitaa, katika mikoa 26 asilimia 45 ya Watanzania walikuwa wamekwishaandikishwa.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na waandiashi wa habari kuhusu uchaguzi wa Serikaliza Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Ameitaja mikoa inayofanya vizuri kwenye uandikishaji kuwa ni Tanga (54.7%), Ruvuma (46.5%), Njombe (45.1%), Songwe (44.6%) na Iringa (40.6%).
Kwa upande wa ile ambayo bado iko chini ya wastani tarajiwa ni Katavi (23.9%), Kilimanjaro (25.1%), Geita (25.5%), Kigoma (26.1%) na Manyara (26.9℅).
Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote Tanzania kufuatilia halmashauri ambazo uandikishaji upo chini na kutatua changamoto zilizobainika ili kwa siku zilizobaki idadi ya watu wanaojiandikisha iweze kuongezeka.
.jpg)
No comments:
Post a Comment