VINCENT MGINA AWAGUSA WANAFUNZI WA KIKE SHULE YA SEKONDARI MADILU.
Mtendaji wa kata ya Madilu Zaveria Mduda kwa kushirikiana na mkazi wa kata hiyo Vincent Mgina wamegawa taulo za kike kwa wanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari Madilu wanaotarajia kuanza mitihani yao ya Taifa ya kujipima ili iwasaidie pale ambapo watakuwa katika mitihani hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi hao oktoba 26 ,2024 Zaveria Mduda amemshukuru mdau huyo kwa kujitoa kwa moyo wote hasa kwakuwagusa wanafunzi hao ,jambo ambalo litaleta hamasa katika kukuza taaluma ya kata hiyo pamoja na kuwafanya wanafunzi kujisikia vizuri wakiwepo shuleni na kuweza kufanya mitihani yao vizuri.



No comments:
Post a Comment