Wafanya Biashara wa Soko Kuu Njombe na soko la wakulima Halmashauri ya mji Njombe wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba.
Akizungumza Disemba 04,2024 Maria Sanga Afisa Elimu kwa Umma kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyada za Juu Kusini na wafanyabiashara hao kuhakikisha wanatumia dawa kwa usahihi kama mtaalamu anavo elekeza dawa hizo.
“Kumekuwepo na wimbi la wananchi kutumia dawa pasipo vipimo vya daktari, kutomaliza dawa kwa muda sahihihi na wengine kutumia dawa za binadamu kwenye mifugo niwaombe mkipata changamoto yoyote ya afya na daktari akakwambia tumia dawa hizi kwa muda wa siku kadhaa tumia muda huo kama ulivyo elekezwa usipofanya hivyo unapelekea usugu wa dawa katika mwili wako na kupelekea dawa hiyo kutofanya kazi katika mwili wako ” Alisema Maria Sanga Kutoka TMDA
Akiendelea Kuzungumza Maria amewataka Vijana na Mabinti ambao wamekuwa wakitumia dawa za nguvu za kiume na Dawa za kuua Mbegu za kiume maarufu (P2) zisitumike kilasiku jambo ambalo linaharibu afya zao kutokana namatumizi mabaya ya dawa hizo kinyume na makusudio yake kwa wananchi hasa kwa ambao wamekutana na changamoto .
“Watu wamekuwa wakitumia P2 kila wakifanyapo tendo la Ndoa lakini kitaalamu inatakiwa zitumike mara 2 kwa mwaka na sio kila wakimaliza tendo la ndoa na kwa wanaume dawa za nguvu za kiume zipo kwa wale ambao wanachangamoto za maumbile yao ya mfumo wa uzazi ,sio kwa watu mbao wazima mnajiua wenyewe vijana achene kuwakomoa mabinti mkiamini dawa za nguvu za kiume zinawaridhisha wanawake hapana!!!!. ” Alisema Maria Sanga Kutoka TMDA.










No comments:
Post a Comment