Wednesday, 4 December 2024

NYUMBA 9 MJI MWEMA NJOMBE ZAEZULIWA NA MVUA KUBWA

 

Katibu tawala Wilaya Njombe Bi. Agatha Mhaiki ametoa pole kwa wakazi wa Mtaa wa Mji Mwema eneo la Msete kwa maaafa ya kuezuliwa nyumba iliyosababishwa  na mvua kubwa iliyo nyesha Disemba 03,2024.











Akizungumza Katibu tawala akiwa eneo la tukio hilo Disemba 04 ,2024 alipoongoza na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Njombe amesema serikali tayari imefanya tathimini kwa nyumba zilizo pata maafa kwa ajili ya ukamilishaji wa Nyumba hizo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Akiendelea kuzungumza na wakazi hao  Mhaiki amesema kwa niabaya ya kamati ya ulinzi na usalama wamechangia shilingi laki tatu tu(300,000)kwa ajili ya wahanga hao huku taratibu zingine za ukusanyaji zikiendelea.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete amsema taratibu za uchangiaji zitaratibiwa na ofisi ya Mtendaji wa kata na Mtaa ili kuhakikisha matumizi ya fedha ambazo watakuwa wamezitoa wadau kutoka maeneo mbalimbali ziwekwe kwenye kwenye  akaunti ya Mtaa ambayo ni  6062300658 -Mtaa wa Mji Mwema ili kuepusha changamoto katika ukusanyaji.

Jumla ya Nyumba 10 Katika Mtaa wa Mji Mwema zimeezuliwa na Mvua kubwa  iliyo nyesha Disemba 03,2024 ambayo ilisababisha maafa hayo.

 

No comments:

Post a Comment

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...