Monday, 9 December 2024

USAFI WAFANYIKA MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA NJOMBE

 Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika Kila Disemba 9 ya mwaka Wananchi mkoani Njombe wameshiriki kufanya usafi wa mazingira na kutoa misaada kwa wagonjwa huku wito ukitolewa kwa jamii kujijengea utamaduni wa kuwa safi wakati wote.


Halmashauri ya mji wa Njombe imesherekea siku hii kwa kufanya usafi katika maeneo ya Kituo cha Afya Njombe mjini,Soko kuu na kupanda miti katika shule ya sekondari Mpechi ambapo Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Njombe mjini Nicodemus Funi anasema pia wamezindua kampeni ya usafi ya siku kumi ndani ya Kata hiyo.



Wenyeviti wapya wa serikali za mitaa ya Kata ya Njombe mjini Akiwemo Malaki Mwandila na Francis Msanga wamesema jamii inao wajibu wa kuweka mazingira sawa wakati wote huku wakitoa vifaa vya usafi katika kituo cha Afya na misaada mingine kwa wagonjwa.

Kwa niaba ya Katibu Tawala wilaya ya Njombe Ofisa Tawala wilaya Bwana Benjamin Machibya ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi Kulinda amani iliyopo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Njombe wamesema usafi unasaidia kukabiliana magonjwa ya mlipuko na ndio maana wameungana na serikali kushiriki zoezi hilo.

Serikali ya Tanzania ilielekeza maadhimisho hayo yafanyike kwa ngazi za mikoa na Wilaya kwa kufanya shughuli za kijamii ambapo mkoani Njombe yamefanyika mabonanza,Usafi pamoja na kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...