![]() |
Wito huo
umetolewa Disemba 04,2024 na Maria Sanga
Afisa Elimu kwa Umma kutoka Mamlaka
ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyada za Juu Kusini ambapo aliwaomba
wakulima na wadau hao wahakikishe wanatumia dawa hizo kama inavyo takiwa kwa
mjibu wa mtaalamu husika ambaye anampa dawa hizo jambo ambalo kwa baadhi ya
watu wanapata usugu wa dawa kutokana na kutumia dawa kwakutozingatia vipimo na
masharti ya daktari.
“Kumekuwepo
na wimbi la wananchi kutumia dawa pasipo
vipimo vya daktari, kutomaliza dawa kwa muda sahihihi na wengine kutumia dawa
za binadamu kwenye mifugo niwaombe
mkipata changamoto yoyote ya afya na daktari akakwambia tumia dawa hizi kwa
muda wa siku kadhaa tumia muda huo kama ulivyo elekezwa usipofanya hivyo unapelekea
usugu wa dawa katika mwili wako na kupelekea dawa hiyo kutofanya kazi katika mwili wako ” Alisema Maria Sanga Kutoka
TMDA
Naye kwa
Upande wake Adam Sorota Mkaguzi wa dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
(TMDA) Kanda ya Nyada za Juu Kusini amewataka wananchi ambao wata kutana
na changamoto watoe taarifa katika kituo
husika walicho pata dawa hiyo au wawasiliane na Mamlaka husika kwa mawasiliano
ya kupiga namba ya simu bila malipo ya 0800 110 084.








No comments:
Post a Comment