MKATABA WA UJENZI WA BARABARA KATA NJOMBE MJINI WASAINIWA.
Katika hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika katika ofisi za Halmashauri ya Mji Njombe Tarehe 11 Novemba 2024, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Erasto Mpete, aliihimiza kampuni hiyo kutekeleza mradi huo kwa ubora na ufanisi ili kufikia matarajio makubwa ya wananchi.“Niwaombe mnapoenda kutekeleza mradi huu, mkazingatie makubaliano tuliyokubaliana katika mkataba, na kuhakikisha kuwa ujenzi unafanyika kwa kuzingatia fedha zilizotengwa,” alisema Mhe. Mpete.Kwa upande wake, Mhandisi Jofrey Dembe kutoka kampuni ya Ubaruku Construction Company Limited aliahidi kutekeleza mradi huo kwa ufanisi na kukamilisha kazi hiyo kwa wakati, kama ilivyoainishwa katika mkataba.Mradi huo utagharimu shilingi milioni 644,423,650 na utahusisha ujenzi wa barabara za Savanna–Hilliside, Sanga–Pombeshop, Pombeshop–Ngailo, na Kivaa–Mgombela.
Blog hii Nikwa ajili ya Habari na Matukio Mbalimbali ya Kijamii pamoja na Habari Mchanganyiko
Wednesday, 13 November 2024
MKATABA WA UJENZI WA BARABARA KATA NJOMBE MJINI WASAINIWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO
WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...
-
Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Njombe TC Wapatiwa Mafunzo ya Lishe Kupunguza Udumavu Njombe, Septemba 10, 2025 – Wahudumu wa afya ngazi ya...
-
Novemba 26, 2025 Maafisa ugani Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji Njombe wamepatiwa mafunzo na Mradi wa YEFFA kuhusu n...

No comments:
Post a Comment