Friday, 27 September 2024

Kitumbua cha Ruto Chaingia Mchanga Kuzua joto la kisiasa Kenya

 


Wiki za hivi karibuni katika siasa za Kenya zimeshuhudia kile kinachoweza kuitwa 'sarakasi' za siasa za Kenya ila inakuwa wazi kwamba kila mambo yanavyobadilika, ndivyo yanavyosalia yalivyokuwa -na hasa katika siasa za taifa hilo la Afrika mashariki.

Naibu wa rais Gachagua sasa anakabiliwa na tishio la kutimuliwa mamlakani kupitia hoja itakayowasilishwa bungeni na washirika wa Rais William Ruto. Katika upande mmoja wa malumbano hayo ni rais na viongozi wa chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA) wanaoumuunga mkono na katika upande wa pili ni naibu wake na viongozi ambao wamesimama naye.

Hatua ya hivi punde inayokashiria kuzorota kwa uhusiano kati ya wawili hao ni ile ya Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kutangaza kwamba serikali itawafungulia mashtaka viongozi kadhaa wanaodaiwa kupanga na kufadhili maandamano ya vijana yaliyotikisa serikali miezi ya Juni na Julai. Wanaohusishwa na njama hizo ni washirika wa Naibu wa Rais.

SOURCE:BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...