Friday, 27 September 2024

WANANCHI NJOMBE WAHIMIZWA KULIMA ZAO LA PARETO

 Na Mario Mgimba 

Njombe

Wananchi Mkoani Njombe wahimizwa kulima zao la Pareto ambalo litawasaidia kuinuka kichumi katika Jamii.

 


Wito huo umetolewa Septemba 24 ,2024 na Mkuu wa Wilaya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa alipokuwa akizungumza na Maafisa Kilimo , Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya Mji Njombe wa maeneo ambayo zao hilo limekuwa likistawi kwa wingi , ambapo Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuchangamkia fursa kutokana na hali ya hewa ambayo inapatikana mkoani njombe kuwa rafiki katika ustawi wa zao hilo la Biashara. 


Kwa upande wake Baraka Mwambene Maratibu Shughuli za Ugani wa zao la Pareto Tanzania amesema zao hilo limekuwa liwasaidia wanachi wengi kujikwimu kimaisha kutokana na bei ya zao hilo kuwa juu katika masoko ya Kimataifa huku faida yake kubwa ambayo inatokana na zao hilo ni kutumika kutengenezea viuatilifu , dawa ya kuulia Mbuu na kusaidia kwenye chakula cha mifugo .


 Zao la Pareto limekuwa likiuzwa kwa shilingi elfu 3500 kwa kilo na kwa ekari moja kunakadiriwa kupandwa miche elfu 22 ambayo ikitunzwa vizuri huzalisha kilo 200 hadi kilo 700 kwa shamba la ekari moja ambazo zikitunzwa vizuri faida yake ni kubwa kupitia zao hilo la Biashara .



1 comment:

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...