Friday, 7 November 2025

Meneja wa Soko Kuu Njombe Aungana na Wafanyabiashara Kufanya Usafi

 Meneja wa Soko Kuu la Njombe, Ndugu Enosy Lupimo, leo tarehe 07 Novemba 2025, ameungana na wafanyabiashara wa soko hilo katika zoezi la kufanya usafi lililofanyika katika eneo la Soko Kuu Njombe. Zoezi hilo limehusisha kusafisha njia kuu za soko, mifereji ya maji machafu pamoja na maeneo ya dampo.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Ndugu Lupimo amesema kuwa lengo la usafi huo ni kuhakikisha soko linabaki katika hali ya usafi na usalama wa kiafya kwa wafanyabiashara pamoja na wateja wanaofika kununua bidhaa mbalimbali.






 “Usafi ni wajibu wa kila mmoja wetu. Tunaposhirikiana, tunaleta mazingira bora ya biashara na afya njema kwa jamii,” amesema Meneja huyo.

Aidha, amewasihi wafanyabiashara kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara ili kulifanya soko hilo kuwa mfano wa kuigwa katika Mkoa wa Njombe.

Wafanyabiashara waliopata fursa ya kushiriki wamepongeza uongozi wa soko kwa kuonyesha mfano wa vitendo na kuahidi kuendeleza

No comments:

Post a Comment

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...