MHE. ANTHONY MTAKA AKUTANA NA
VIONGOZI WA DL GROUP NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA NJOMBE
Mkuu wa Mkoa wa
Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Kampuni ya DL Group, Ndugu Dr. David Langat, pamoja na viongozi wa
wafanyabiashara kutoka mkoa wa Njombe.
Katika kikao hicho walihudhuriwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali za mkoa, pamoja na vikundi vya uwakilishi kutoka kwa wanawake.
![]() |
Kikao Hicho
Kilijikita katika kujadili fursa za
uwekezaji katika viwanda, na namna ambavyo sekta hii itakavyoinua uchumi wa
wananchi wa Njombe. Fursa za uwekezaji zilijikita katika zao la parachichi,
chai, na viazi, ambapo kupitia uwekezaji katika viwanda vya usindikaji, kuna
matumaini ya kuongeza mnyororo wa dhamani wa mazao haya na kuleta manufaa kwa
wakulima na wajasiriamali wa eneo hili.
Mhe. Mtaka
alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na sekta binafsi ili kuleta maendeleo ya
kiuchumi kwa wananchi wa Njombe, huku akitaja kuwa uwekezaji huu utasaidia
kuongeza ajira, kuboresha miundombinu, na kukuza sekta ya kilimo. Wadau
walieleza matumaini yao kwamba hatua hizi zitakuza uchumi wa mkoa na kuboresha
hali ya maisha ya wakazi wake.








No comments:
Post a Comment