Thursday, 24 July 2025

Viongozi Wapya wa Tiba Asili Njombe Wachaguliwa Njombe TC

 

 

Viongozi Wapya wa Tiba Asili Njombe Wachaguliwa Njombe TC

 







Njombe,

Julai 23, 2025 –Kundi la wataalamu wa tiba asili wakiongozwa na Dkt. Kusulila, ambaye pia ni Katibu wa Tiba Asili nchini na Mratibu wa magonjwa ya kifua kikuu na Ukimwi, Halmashauri ya Mji Njombe limefanya kikao maalum katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, ambapo viongozi wapya wa kundi hilo walichaguliwa rasmi.

 

Kikao hicho kilihudhuriwa na waganga wa tiba asili kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya mji njombe na kuwezeshwa na uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, chini ya Katibu wa Halmashauri hiyo. Kikao kililenga kuimarisha mwelekeo wa huduma za tiba asili sambamba na kanuni za kiafya na maadili ya taaluma hiyo.

 

Dkt. Kusulila alieleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na mifumo ya usimamizi thabiti kwa waganga wa tiba asili, ili kuhakikisha wanatoa huduma salama na zinazozingatia taratibu za afya. Alisisitiza kuwa tiba asili inapaswa kushirikiana na huduma za kisasa, hasa katika mapambano dhidi ya magonjwa sugu kama Ukimwi na kifua kikuu.

 

“Tunataka kuondoa matabibu wa kiholela na kuhakikisha kila mganga wa tiba asili anasajiliwa, anapata mafunzo, na anashirikiana na sekta rasmi ya afya. Hii itasaidia kulinda wananchi dhidi ya madhara na kukuza tiba asili kwa njia ya kitaalamu,” alisema Dkt. Kusulila.

 

Kwa upande wake, Katibu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe alitoa wito kwa waganga wa tiba asili kufanya kazi kwa kushirikiana

na serikali na kuzingatia sheria. Aliahidi kuwa halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa kuhakikisha kuwa huduma za tiba asili zinatambuliwa na kusimamiwa ipasavyo.

 

Viongozi walioteuliwa katika kikao hicho watawajibika katika kusimamia usajili wa waganga, nidhamu, na kuandaa mikakati ya maendeleo ya tiba asili kwa mkoa wa Njombe.

No comments:

Post a Comment

AKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO

  WAKULIMA WA CHAI NJOMBE WAIBUA CHANGAMOTO ZA MIUNDOMBINU NA SOKO Wakulima wa zao la chai mkoani Njombe wameiomba serikali pamoja na wada...